Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TUPO TAYARI KWA LIGI KUU-LOGARUSIC

Kocha wa klabu ya Simba Zdravko Logarusic 'Loga' amesema kuwa hana shaka na kikosi chake na kwa sasa timu yake ipo tayari kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara.

Akizungumza jana, Loga, alisema kuwa michezo ya kombe la mapinduzi imewaimarisha zaidi wachezaji wake na kwa sasa wanasubiri mzunguko wa pili wa ligi kuu.

Alisema kuwa wachezaji watakaopata nafasi kwenye mzunguko wa pili wa ligi ku ni wale watakaoonyesha uwezo.

"Mechi tulizocheza Zanzibar zimetumarisha zaidi ni maandalizi mazuri kwa ajili ya ligi..., sina shaka na timu yangu kwa sasa tupo tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu," alisema Loga.


Alisema kuwa lengo lake ni kuhakikisha Simba inachukua ubingwa msimu huu na kusisitiza kuwa uwezo wa kufanya hivyo wanao.

"Nina wachezaji wenye uwezo mkubwa... kila mchezaji akitimiza majukumu yake nina uhakika wa ubingwa mwisho wa msimu," aliongezea kusema Loga.

Alisema kuwa kwake yeye kila mchezaji anauwezo mkubwa lakini navutiwa zaidi na mchezaji Ramdahani Singano 'Messi'.

"nataka wachezaji wajitume kama anavyofanya yeye (Singano), amekuwa mfano wa kuigwa najituma na anajua kazi yake," aliongezea kusema Loga.

Aidha, Kocha huyo aliema mchezo wa kirafiki wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar angependa uwe wa mwisho na wajipange kwa ajili ya mzunguko wa pili.

Simba leo inacheza na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa kirafiki ikiwa ni sehemu maandalizi ya timu hizo kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu uliopangwa kuanza Januari 25.

Simba inacheza na Mtibwa huku ikiwa imetoka kushiriki mashindano ya kombe la mapinduzi ambapo wamefanikiwa kushika nafasi ya pili baada ya kufungwa goli 1-0 kwenye mchezo wa fainali na KCCA ya Uganda.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa