YANGA KUTUPA KARATA NYINGINE LEO UTURUKI, KUCHEZA NA TIMU YA LIGI KUU.

Mabingwa wa soka nchini, Yanga wanaendelea na mandalizi yao kwa ajili ya ligi kuu na mashindano ya kimataifa na leo wanacheza mchezo wa tatu wa kirafiki dhidi ya KS Flamurtari Vlore inayoshiriki ligi kuu nchini  Albania.

Yanga ipo nchini Uturuki ilipokwenda kuweka kambi na itacheza na timu hiyo ambayo nayo ipo nchini humo kwa ziara ya mafunzo.

Akizungumza kwa njia ya simu, Afisa Habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, alisema kuwa mchezo huo wa leo ni sehemu ya mafunzo yao na kocha mpya wa timu hiyo, Johanes Franciscus 'Hans' van der Pluijm anataka kutumia michezo ya kirafiki nchini humo kukifahamu vizuri kikosi chake.


"Mwalimu anatumia michezo hii kuwaona wachezaji wake kama unavyojua ameungana na timu hivi karibuni tu, hii ni nfasi yake ya kuangaliwa wachezaji wake ili ajue anaanzia wapi," alisema Kiziguto.

Alisema timu hiyo ilifanya mazoezi ya nguvu juzi asubuhi chini ya kocha mpya na wako tayari kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki.

Alisema kuwa baadea ya mchezo wa leo watacheza mchezo mwingine wa kirafiki katikati ya wiki ambao utakuwa wa msiho kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini.

Aidha, alisema kuwa kambi ya timu hiyo aina majeruhi zaidi ya kiungo, Hassan Dilunga ambaye anasumbuliwa na malaria.

"Dilunga anasumbuliwa na malaria lakini tayari ameanza dozi na anatibiwa na daktari wa timu Suphian.., zaidi ya huyo hakuna majeruhi mwingine," alisema kiziguto.

Alisema kuwa kambi ya nchini humo imewasaidia zaidi wachezaji wake ambao sasa wapo tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara.

Ikiwa nchini humo tayari Yanga imecheza michezo miwili ya kirafiki na zote kuibuka na ushindi

Awali ilianza kucheza na Ankara Sekerspor na kushinda magoli  3-0 na baadae kucheza na Altay Sk na kuibuka na ushindi wa magoli 2-0.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA