YANGA WAIPANIA COASTAL UNION.

Na Elias John

MABINGWA wa soka Tanzania bara Yanga, wameonyesha kuipania Coastal Union ya Tanga watakayokutana nayo keshokutwa jumatano kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga, Timu hizo ambazo zote zilikuwa nje ya nchi wakati zikijiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu bara zinakutana katika mchezo wa marudiano baada ya kutoka sare katika mechi yao ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa Yanga wamesema watacheza kufa na kupona ilikuondoka na pointi tatu katika mchezo huo,David Luhende ambaye kwa sasa anacheza kamakiungo wa pembeni ametamba ni lazima Yanga iibuke na ushindi katika mchezo huo ili kuendelea kuongoza ligi.

'Nimeipania sana Coastal, ni lazima tujitume ili tuambulie pointi tatu' alisema Luhende,Luhende ambaye katika mchezo wa kwanza uliofanyikja uwanja wa Taifa alisababisha penalti iliyozaa bao la kusawazisha la Coastal Union ambalo lilileta tafrani na kupelekea basi lililobeba wachezaji wa Coastal kupigwa mawe na mashabiki wa Yanga.


Naye mshambuliaji hatari wa Yanga Didier Kavumbagu yeye ameahidi kutoka na goli katika mchezo huo, mechi hiyo inatajwa kuwa na ushindani wa aina yake hasa kutokana na timu hixoxinapokutana huwa zinakamiana, Yanga na Coastal zilirejea nchini hivi karibuni ambapo zote zilifanya ziara nje ya nchi.

Yanga ilikwenda Uturuki wakati Coastal Union ilifanya ziara yake Oman, timu hizo zilianza mechi zake za kwanza mzunguko wa pili mwishoni mwa wiki iliyopita ambapoYanga ilianza vema kwa kuilaza Ashanti United mabao 2-1, huku Costal Union ikilazimishwa sare na JKT Oljoro ya Arusha. 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA