MESSI HAUZWI, ASEMA BARTOMEU.
Kuna uvumi kuwa Messi ambaye ni mshindi mara nne wa tuzo la Ballo d'Or, mwenye umri wa miaka 26, analengwa na kilabu ya Ufaransa ya Pris St-Germain.
Lionel Messi ameshiriki pakubwa katika kusaidia Barcelona kufunga zaidi ya mabao 36 katika msimu huu na amekuwa katika kikosi cha ushindi mara 16 ati ya michezo 20 iliyochezwa.
Katika mahojiano na kituo cha radio cha RAC1, yaliyonukuliwa katika mtandao wa Barcelona, Bartomeu anasema: "Kilabu kitaketi na kushauriana mkabala mpya. Tutafanya kila tunaloweza kuhakikisha kuwa yeye ndiye mchezaji anayelipwa mshahara bora zaidi."
Messi alipachika wavuni mabao 60 katika mechi 50 alimoshiriki katika msimu uliopita Messi lakini kwa sasa anajitahidi kufikisha mabao kama hayo msimu huu wa mwaka 2013-14.
Hadi kufikia sasa amefunga mabao 18 na manane kati ya hayo ndiyo aliyoyafunga katika Ligi, ingawa amesaidia kufunga mabao 36 katika mechi 20 alimoshiriki.