Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KAPOMBE KUREJEA SIMBA.

Uongozi wa klabu ya Simba umesema endapo beki, Shomary Kapombe, atashindwa kurejea AS Cannes inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Ufaransa, mchezaji huyo atalazimika kurejea katika klabu hiyo na hayatatokea kama yalivyojitokeza kwa aliyekuwa mshambuliaji wao, Emmanuel Okwi.

Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zimeeleza kwamba Kapombe hataki kurejea Ufaransa licha ya madai yake dhidi ya klabu hiyo kutatuliwa.

Akizungumza na jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alisema kwa sasa Kapombe ni mali ya wakala, Denis Kadito na kama kuna matatizo kati yake

na wakala huyo wanatakiwa kukaa na kuzungumza ili kutimiza makubaliano waliyoingia kabla ya kujiunga na AS Cannes.

Rage alisema wanaamini Kapombe bado ana nafasi ya kupata klabu barani Ulaya na atakapofanikiwa itakuwa ni faida kwa mchezaji husika na nchi pia.


Mwenyekiti huyo, alisema endapo Kapombe ataamua kuikacha AS Cannes atatakiwa kurejea nchini kuitumikia Simba kwa sababu ana mkataba unaomalizika 2016.

“Wala haitatokea kama ilivyokuwa kwa Okwi, hata sisi tunashindwa kuzungumza na Kapombe kwa sababu tunazifahamu kanuni na taratibu za Fifa, sasa hivi mchezaji yule ana wakala na yeyote anayemhitaji anatakiwa kupitia kwa wakala na si kinyume na hapo,” Rage aliongeza.

Alieleza baadhi ya makubaliano yaliyopo kati ya mkataba wa Kapombe na wakala, Simba itapata asilimia 20 mchezaji huyo atakapouzwa katika klabu nyingine au atarejea

kuitumikia Wekundu wa Msimbazi endapo atashindwa kupata timu huko Ulaya.

Kapombe ambaye alisajiliwa na Simba akitokea Polisi Morogoro, mkataba wake wa awali na Simba ulikuwa unatarajiwa kumalizika Aprili mwaka lakini mwaka jana klabu

hiyo ilimuongezea mkataba wa miaka miwili na kumuongezea mshahara wake yeye pamoja na wachezaji wengine waliopandishwa kutoka Simba B.

Beki huyo yuko hapa nchini tangu mwaka jana na habari zaidi zinaeleza kuwa, klabu za Yanga na Azam zinadaiwa kufanya mazungumzo ya awali ya kutaka kumsajili.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa