MAN UNITED SASA NYOKA WA KIBISA.

David Moyes ameendelea kuwanyima raha mashabiki wa Manchester United, baada ya usiku wa jana timu hiyo kutolewa katika Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, kwa penalti 2-1 kufuatia sare ya jumla ya 3-3 Uwanja wa Old Trafford, Manchester, England.

Sunderland ilishinda 2-1 katika mchezo wa kwanza nyumbani na leo ikalala 2-1 baada ya dakika 120. Evans alianza  kuifungia United dakika ya 37 na bao hilo likadumu hadi dakika 90 ndipo zikaongezwa dakika 30 na Bardsley akaisawazishia Sunderland dakika ya 119.


Javier Hernandez 'Chichari' akaifungia United bao la pili dakika ya 120 na ushei na mchezo ukahamia kwenye matuta. Upande wa Man United Darren Fletcher pekee alifunga penalti, wakati Welbeck, Januaj, Jones na Rafael wote walikosa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA