COASTAL UNION WABEBA NDOO OMAN BAADA YA MIAKA 26.

 MARA ya mwisho Coastal Union ya Tanga kushinda taji ilikuwa ni mwaka 1988 walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wakati huo ikiitwa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Tangu wamekabidhiwa Kombe la ubingwa wa Bara, Coastal hawajawahi kukabidhiwa taji lingine kwa sababu hawajashinda mashindano yoyote mengine baada ya hapo.

Lakini jana, ikiwa ni miaka 26 baadaye, timu hiyo ilipewa taji, baada ya kukabidhiwa Ngao ya Urafiki na klabu ya Fanja ya Oman, kutokana na kuzuru nchini hapo kucheza mechi ya kirafiki na klabu hiyo kigogo.


Mwenyekiti wa Coastal, Ally Hemed ‘Aurora’ alikuwa mwenye tabasamu pana wakati anapokea Ngao hiyo kutoka kwa Mwenyekiti wa Fanja, Saif Al Sumry.  Mataji matamu, lakini lazima wayapiganie uwanjani.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA