EMMANUEL OKWI ANUKIA MSIMBAZI
MGANDA Emmenuel Okwi aliyesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili na nusu kukipiga Yanga kabla na shirikisho la kandanda nchini TFF kuingilia kati kuhoji usajili wake kama una baraka zozote kutoka Fifa, Imebainika kuwa mchezaji huyo atarejeshwa katika klabu yake ya zamani ya Simba endapo klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia itashiondwa kuilipa Simba SC pesa zake dolaza Kimarekani 300,000.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ambaye ni rafiki wa karibu na mjumbe mmoja wa kamati ya sheria, hadhi za wachezaji wa TFF amedai kuwa barua iliyoandikwa na TFF kwenda Fifa ilikuwa na nmaaguizo mawili tu.
Agizo la kwanza ni kutaka kujua kama kweli Okwi ana uhalali wa kukipiga Yanga, wakati la pili likitaka klabu ya Simba ilipwe pesa zake za usajili ama sivyo Simba irejeshewe mchezaji wake harafu imuuze kwa timu nyingine kama itataka au aendelee kuichezea.
Endapo Fifa itaamua kupitisha mapendekezo hayo mawili ya TFF basi mchezaji huyo atarejea katika klabu yake ya zamani ya Simba na kuifanya Yanga ichanganyikiwe, Yanga ilitangaza kumnunua Okwi kutoka klabu ya SC Villa ya Uganda ambayo nayo ilipewa kwa mkataba wa miezi sita na Fifa baada ya klabu yake ya Etile Du Sahel kushindwa kumlipa mshahara wa miezi mitatu.
Hata hivyo chanzo hicho cha habari kimesema kwamba bado Fifa inaendelea kupitia mapingamizi matatu ya mchezaji huyo na ikijiridhisha itatoa tamko, 'Inawezekana akaruhusiwa kuicheza Yanga au kumrejesha katika klabu yake ya zamani', kilisema chanzo hicho.