RONALDO KUWANUNULIA GARI JIPYAAAA MADAKTARI REAL MADRID...NI FURAHA YA BALLON D'OR
NI kazi ngumu kuwa mchua misuli wa Cristiano Ronaldo, lakini wakati mwingine inalipa.
Mchezaji
huyo ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia,
FIFA Ballon d’Or amewaahidi madaktari wa Madrid kuwanunulia gari mpya
baada ya kushinda tuzo hiyo wiki hii.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na Sportsmail,
kocha wa Real Madrid, Paul Clement amezungumzia mambo ambayo Ronaldo
atayafanya atakaporejea kutoka kwenye mechi za katikati ya wiki za Ligi
ya Mabingwa.
Ronaldo alimwaga machozi wakati anapokea tuzo hiyo. Kulia ni Pele.
Kocha Msaidizi wa Madrid, Paul Clement (kushoto) akiwa na Zidane
Ronaldo
anatambua na kuheshimu sana mchango wa madaktari wake na wakati wote
amekuwa mkweli wa ahadi kwao na awali amekwishawahi kuwazawadia saa mpya
na simu aina ya iPhones toleo jipya.
Wote kazini! Ronaldo alipigwa picha akifanyiwa massage na timu nzima ya madaktari wa Madrid mwezi uliopita