UNYAMA MTUPU: KIJANA AUAWA MCHANA KWEUPEE, AHUSISHWA NA 'UASI' TABATA.
HALI imeanza kuwa mbaya hasa jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake, wananchi wenye hasira kali waishio Tabata Mtambani wamempiga mpaka kumuua kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Shada Ibada (Pichani) kwa kumuhusisha na kundi l.akiharifu linalofahamika kwa jina la 'Waasi' ambalo kwa sasa limekuwa kero katika maeneo hayo.
Mwandishi wa habari hizi ambaye alikuwa shuhuda wa tukio hilo amedai kuwa marehemu alikuwa akisakwa kwa muda mrefu kutokana na kujihusisha kwake na vitendo vya uharifu, kabla ya kuuawa marehemu alituhumiwa kuiba maeneo ya jirani ndipo alifukuzwa na wananchi wenye hasira na kumshushia kipigo kilichopelekea kifo chake.
Tayari mwili wa marehemu umeshachukuliwa na polisi na kupelekwa hospitali kwa kuhifadhiwa, hivi karibuni kumezuka kwa vikundi vya vijana vinavyojhihusisha na uporaji, ubakaji na kuharibu amani ya watu, wakazi wa Tabata nao wamejikuta wakiishi kwa shida kufuatia kikundi cha 'Waasi' kuanzisha mtindo mchafu wa uporaji na ubakaji.
Kikundi hicho kimekuwa kikifanya uharifu huo kwenye shughuri mbalimbali hasa sherehe ambapo nyakati za usiku hujitokeza na kuanza uporaji wao, watu mbalimbali wamejitokeza kulaani vikali mchezo mchafu unaofanywa na kikundi hicho cha uasi.
Hata hivyo kampeni imeanzishwa na wakazi wa maeneo hayo ya kuwakamata nyumba hadi nyumba vijana wanaojihusisha na mchezo huo, Jitihada zao zimeungwa mkono na jeshi la polisi ambapo hadi sasa vijana zaidi ya 10 wameshafikishwa polisi huku wengine wakiendelea kusakwa.