ETO'O KUENDELEA KUTESA CHELSEA

Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, ametangaza kuna uwezekano nyota wa Cameroon, Samuel Eto’o, atasalia katika klabu hicho msimu ujao licha ya habari anakusudia kurejea Uhispania kandarasi yake itakapoisha Juni.

Mourinho anakusudia kumhifadhi mshambulizi huyo wa zamani wa Mallorca na Barcelona, 32, lakini anasema uamuzi wa mwisho uko mikononi mwa klabu ama Eto’o musimu utakapo karibia kuyoyoma.

Eto’o ameibuka mshambuliaji kigezo wa timu hiyo huku Fernando Torres akiendelea kuuguza jeraha la goti huku kampeni ikizidi kuchacha moto.


“Tuna uhusiano wa kuaminiana naye na amefikia wakati wa mchezo wake ambao yuko huru kufanya maamuzi yanayomhusu. Amefutahia kuwa hapa kwani dhamira yake ni kungangania mataji.

“Tutaona ni nini analotaka kufanya mwisho wa musimu. Pengini ni kurejea Mallorca kama alivyoahidi mwanawe, pengine ni kusalia hapa au kumaliza mchezo wake wa kulipwa Inter Milan,” Mourinho aliongeza.

Eto’o amezamisha mabao manane tangu kujiunga na Chelsea kutoka timu ya Urusi ya Anzhi Makhachkala, yakiwemo matatu dhidi ya mabingwa wa Uingereza, Manchester United, yalioonekana kuzima utetezi wa taji lao.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA