Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SIMBA YATISHA ZANZIBAR, YATINGA FAINALI KWA KISHINDO.

SIMBA SC wamefuzu kuingia Fainali ya Kombe la Mapinduzi, baada ya jana usiku kuilaza mabao 2-0 URA ya Uganda kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Shujaa wa Simba SC jana alikuwa ni kiungo mwenye kipaji, Amri Ramadhani Kiemba aliyesababisha bao la kwanza na kufunga mwenyewe la pili.

URA ilipata pigo mapema dakika ya 32 baada ya mshambuliaji wake hatari, Owen Kasule kutolewa nje kwa nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu winga msumbufu wa Simba SC, Ramadhani Singano ‘Messi’.


Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika timu hizo zikiwa hazijafungana na kipindi cha pili ndipo Simba SC inayofundishwa na Mcroatia, Zdravko Logarusic ilipofungua makucha yake.
  
Kona maridadi ya Kiemba ilimkuta beki Donald Mosoti, aliyemsetia beki pacha wake wa kati, Joseph Owino akafunga bao la kwanza dakika ya 49.

Wakati URA wanahaha kusaka bao la kusawazisha, Simba SC walifanya shambulizi zuri na krosi maridadi ya Haroun Chanongo ikaunganishwa nyavuni na Amri Kiemba dakika ya 52 kuipatia Simba SC bao la pili.

Bao hilo liliinyong’onyesha kabisa URA, ingawa iliendelea kupambana kupata japo bao la kufutia machozi.

Kwa ujumla, URA iliathiriwa mno na kutolewa na mshambuliaji wake hatari, Owen Kasuule, kwani ndiye tegemeo lake la mabao kwa pamoja na Feni Ali.

Baada ya mechi, Kiemba alipewa king’amuzi cha Azam TV kwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

Simba SC sasa itapambana na KCC ya Uganda pia katika Fainali Jumatatu Saa 10:00 Uwanja wa Amaan.

Ikumbukwe Simba na KCC zote zimetokea Kundi B na katika mechi baina yao, zilitoka sare ya bila kufungana.

Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’/William Lucian 'Gallas', Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haroun Chanongo, Amri Kiemba/Said Ndemla, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amisi Tambwe/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ na Awadh Juma/Uhuru Suleiman.

URA; Mugabi Yassin, Samuel Ssenkoom, Alan Munamba/James Kasibante, Mussa Doca, Jonathan Mugabi, Oscar Agaba, Augustine Nsumba, Owen Kasuule, Erisa Sekisambu/Ngama Emmanuel, Feni Ali/Milos Ilic na Hashimu Sempalia.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa