LOGARUSIC APANIA KUIVURUGA YANGA YA 'KIBABU'

Kocha wa Simba, Zdravco Logarusic amesema hawezi kupoteza muda kwa kupigana vijembe na kocha wa Yanga, Mdachi Hans Van Der Pluijim, atamshushia heshima kwa kuhakikisha anatwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Akizungumza na Mtandao huu, Logarusic  alisema ujio wa Pluijm haumpi tabu, kwa vile mechi aliyopoteza wakati akiifundisha Ashanti Gold ya Ghana haikuwa ya mashindano rasmi bali  maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya nchini humo.

“Nataka ufahamu kwanza imepita miaka mitatu tangu tulipokutana na mimi kupoteza mchezo, ni muda mrefu sana umepita  siyo jana.


“Nakumbuka  haikuwa mechi ya  ligi, ilikuwa mechi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi, msimu wa 2011-12 mimi nilimaliza ligi katika nafasi ya pili, lakini alifanya vibaya na akafukuzwa,” aliongeza:

“Nawaomba mashabiki wasisumbuke sana wasubiri mwisho wa msimu, pale ndiyo sehemu mwafaka ya kutoka hukumu, lengo langu ni kutwaa ubingwa, sina muda wa kutupiana  maneno na  tukikutana nitamfunga.”

Licha ya kauli yake hiyo, Logarusic aliipongeza Yanga kwa kusema imefanya uchaguzi sahihi kumtwaa Pluijm ambaye  alimwelezea kama kocha mwenye uzoefu na utashi mkubwa katika soka.

“Ninaweza kusema Yanga imefanya uteuzi sahihi, kama itamtumia vizuri Pluijm ni kocha mzoefu na mwenye utashi mkubwa katika kazi ya kufundisha soka,”.

Kwa mujibu wa msimamo wa ligi kuu Ghana msimu wa 2011-12, Ashanti Gold iliyokuwa inanolewa na Logarusic ilikamata nafasi ya pili baada ya  kujikusanyika pointi 49 nyuma ya Asante Kotoko iliyotwaa ubingwa ikiwa na pointi 63, wakati Belekum Chelsea ya Pluijm ilimaliza ligi ikiwa katika nafasi ya saba za pointi zake 45.

Hivi karibuni, Pluijm akizungumza baada ya kutangazwa kuwa kocha mpya wa Yanga akirithi mikoba ya  Ernest Brandts aliyetimuliwa, alisema anazifahamu vizuri mbinu za Lugarusic hivyo atatumia fursa hiyo kumchachafya.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA