ADEBAYOR AZIDI KUNG' ARA LIGI KUU ENGLAND
Emmanuel Adebayor alifunga mawili na kusaidia Tottenham kuwatoa wenyeji Swansea manyoa 3-1 kuendeleza matokeo bora chini ya utawala mpya wa meneja Tim Sherwood.
Mshambuliaji huyo wa Togo alisaidia klabu chake kuandikisha alama sawa na Liverpool walioko nafasi ya nne huku Sherwood akisherehekea ushindi wa tano na sare moja katika ligi ya Premier baada ya kumrithi Andre Villas-Boas.
Swansea walisalia alama tatu mbele ya eneo la hatari baada ya kuenda mechi nane bila ushindi.
Adebayor alipata la ufunguzi kati ya kipindi cha kwanza pale alipozamisha krosi safi kutoka kwake Christian Eriksen.
Chico Flores alipata mkosi wa kujifunga pale alipoelekeza krosi ya Kyle Walker wavuni mwao dakika nane baada ya kipindi cha pili kuanza.
Adebayor alihakikisha ushindani dakika 20 kabla ya kipenga cha mwisho kuandikisha lake la tano katika mechi sita za Premier.
Wilfried Bony alifanikiwa kupatia wenyeji bao la kusitiri msiba dakika zikizidi kukatika.