MAKALA: DINO MANYUTI, NYOTA MPYA BONGOFLEVA ANAYETAMBA NA TAM TAM.

Na Exipedito Mataruma

Kizazi kipya ndani ya bongofleva, apania na wimbo wake Tam tamNi kijana mdogo anayetokea kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kwa sasa na wimbo wake wa Tam tam ambao umeanza kupata wafuasi wengi.

Kutamba kwa wimbo wake huo kunaweza kumfanya afikie dhamila yake ya kujulikana na kuweza kupata mafanikio kama ilivyo kwa nyota wengine wa muziki huo wa kizazi kipya.

Bila shaka mbuyu ulianza kama mchicha, hata masupa staa wa sasa kama Naseeb Abdul maarufu Diamond Plutinum, Ommy Dimpoz, Rich Mavoko, Ay na wengineo hawakuanza kujulikana ghafra, walitumia muda wao mpaka kufahamika na sasa wanafaidi matunda ya muziki.

Abdalah Ramadhani Manyuti a.k.a 'D Sina shaka' (Pichani) ameanza kupata unafuu baada ya kusota kwa muda mrefu kwenye muziki huo bila mafanikio yoyote, Kijana huyo anaweza kufikia nyendo za wakali wengine wa muziki huo.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Manyuti alisema kwamba alianza muziki tangia mwaka 2005, 'Nilianza muziki toka mwaka 2005 ila rasmi nilianza kurekodi mwaka 2007 'Pasu kwa Pasu studio Ludigo ndio prodyuza wa kwanza kunitengenezea wimbo', alisema na kuongeza.

'Nikafanya ngoma studio moja inaitwa Kama kawa rekord kwa Marco Chali alikua prodyuza wangu wa pili, ikaja mwaka 2009 nikafanya ngoma studio nyingine inaitwa Kazi One Record ilikuwa mwaka 2010 ndio nikawa rebo Burn record iliyo chini yake Sheddy Clever.

Mwaka 2013 mwezi wa 12 nikakutana na Sabi Sam ambaye ndiye bosi wangu wa sasa tukafungua studio inayoitwa Rash Records tukatengeneza ngoma ya kwanza iitwayo Tam tam, prodyuza anaitwa Naroh na ndio ngoma ambayo ipo redioni kwa sasa', alisema na kuongeza.

'Tumeshafanya video, video yenyewe nikali sana imefanywa na Raymond Kasogaa 'The dream videos'  malengo yangU ni kuufanya muziki wangu uwe wa kimataifa nahitaji kufanya mapinduzi makubwa kwenye muziki wetu wa bongo fleva, sasa hivi nipo chini ya Rash Ent chini ya mkurugenzi Sabi Sam na meneja maneno Mr Project watanzania wakae mkao wa kula kwani nimepania kufanya makubwa sana kwenye muziki wetu wa Tanzania', alimaliza Manyuti.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA