AZAM YAVULIWA RASMI UBINGWA WA MAPINDUZI.
Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC jana walivuliwa ubingwa baada ya kukubali kipigo cha magoli 3-2 kutoka kwa KCC ya Uganda kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan kisiwani hapa.
Azam ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa nyota wa mchezo huo, ‘yoso’ Joseph Kimwaga katika dakika ya 16 akimalizia kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na beki wa pembeni Erasto Nyoni.
Azam waliendelea kuliandama goli la KCC na katika dakika ya 32 kimwaga tena aliipatia Azam goli la pili akimalizia kwa mguu wa kulia pasi ya ‘kupenyeza’ iliyopigwa na Kipre Tchetche baada ya raia huyo wa Ivory Coast kuwachambua mabeki wa KCC kabla ya kutoa pasi hiyo kwa mfungaji.
Hata hivyo dakika tano baadae, KCC walipata goli la kwanza lililofungwa na beki wake Ibrahim Kiiza kwa shuti kali la mguu wa kushoto lililotokana mpira wa faulo uliomshinda mlinda mlango wa Azam Mwadini Ali.
Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko Azam ilikuwa mbele kwa goli 2-1.
Kipindi cha pili cha kilianza kwa kasi huku KCC wakionekana kutafuta goli la mapema ambapo juhudi zao zilizaa matunda dakika sita tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili ambapo Tony Odur aliisawazishia KCC kwa kufunga goli zuri akimalizia pasi ya mfungaji wa goli la kwanza Kiiza.
Huku ikionekana kama mchezo huo utamalizika kwa sare, KCC waliwashangaza Azam baada ya winga wake wa kushoto William Wadir kuiandikia timu yake goli la tatu na la ushindi baada ya kuwakimbiza kwa kasi mabeki wa Azam kabla ya kuachia shuti kali liloshinda golikipa Mwadini ambaye alikuwa ametoka golini kwenda kumzuia winga huyo.
Baada ya mchezo huo, Kocha msaidizi wa Azam FC, Kally Ongala, alisema kuwa wachezaji wake ‘walitoka mchezoni’ baada ya kufungwa goli la pili.
Alisema kuwa wapinzani wao walitumia makosa hayo na kupata goli la ushindi.
Kwa upande wake, Kocha wa KCC, George Nsimbe, alisema kikosi chake kiliizidi mbinu Azam hasa kipindi cha pili kutokana na uzoefu wa wachezaji wake.
Kwa matokeo hayo, KCC imetinga hatua ya fainali na ilikuwa ikisubiri mshindi wa mchezo wa jana usiku kati ya Simba na URA kuungana kucheza fainali ya mashindano hayo itakayochezwa kesho Jumapili.