MOYES SASA KUSAJILI NYOTA WAPYA.
David Moyes, ambaye anazidi kuzingirwa na matatizo chungu mzima kwenye utawala wake mchanga Mancheter United amekiri anahitaji kununua nguvu mpya kwa dharura katika soko la Januari.
Lakini mwalimu huyo pia alikubali kuwa hilo linaweza kutibuka kutokana na hali wasi wasi ya kifedha katika mabingwa hao wa Ligi ya Premier ya Uingereza.
Moyes alikuwa anazungumuza muda mchache baada ya kushuhudia vijana wake wakingatuliwa kutoka Kombe la FA na Swansea waliowanyoa 2-1 nyumbani kwao Old Trafford Jumapili.
“Nitajaribu lakini ninashauku kuwa naweza leta wachezaji wapya hapa Januari. Kuna dharura ya kusajili viungo wapya lakini swali ni, watapatikana?
“Hakuna haja ya kusema mengi kwani wachezaji tunaotamani huenda wasipatikane Januari,” Moyes alisema baada ya United kushindwa kwa mara ya nne nyumbani ndani ya mechi sita.
Washambuliaji matata, Wayne Rooney na Robin Van Persie, walikosa mechi hiyo huku mlinda ngome Rio Ferdinand akiumia na Fabio aliyechukuwa mahala pake kupewa kadi nyekundu.
Hata hivyo, Moyes alikataa kulaumu matokeo hao kwa kukosa huduma za viungo wake muhimu.
“Tulikuwa na kikosi cha nguvu chenye viungo wa kimataifa isipokuwa pengine Alex Buttner.
“Ni lazima tupate jawabu la ushindi, hilo ni mmoja ya majukumu yangu. Haijalishi tutatumia mbinu gani lakini ni lazima tusake vile tutarejelea kutamba tena.”
Timu hiyo ina nafasi ya kujisimamisha tena Jumanne pale watakapokabiliana na Sunderland katika awamu ya kwanza ya semi-fainali za Kombe la Ligi.