CHELSEA YAKUBALI KUMUUZA JUAN MATA KWA MAHASIMU WAO.
Ofa ya Manchester United ya £37 milioni ya kumnunua kiungo wa kati Juan Mata imekubaliwa na wapinzani wao katika Ligi ya Premia Chelsea, gazeti la Uingereza la Daily Telegraph liliripoti Jumatano.
Gazeti hilo lilisema Mata alikubaliana na klabu hiyo kuhusu matakwa ya kibinafsi na kwamba angefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu Alhamisi.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania amekuwa akihusishwa na kuhama Stamford Bridge baada ya kushindwa kupata nafasi ya kuanza chini ya meneja Jose Mourinho.
Mchezaji huyo wa miaka 25 amekuwa hapati muda wa kucheza, huku Mourinho akipendelea Wabrazil Oscar na Willian na Mbelgiji Eden Hazard.
United chini ya meneja David Moyes inatafuta nguvu mpya kuimarisha kikosi baada ya mwanzo mbaya kwenye msimu kuacha klabu hiyo ikiwa nambari saba kwenye Ligi ya Premia na alama 14 nyuma ya viongozi Arsenal.
Ada hiyo itavunja rekodi ya United ya kununua wachezaji ambayo ilikuwa ni ya ununuzi wa Dimitar Berbatov, aliyejiunga nao 2008 kutoka Tottenham Hotspur kwa £30.75 milioni.
Mourinho amekuwa akisisitiza kwamba Mata bado ana jukumu la kutekeleza Chelsea, lakini kujitolea kwake kukwamilia mchezaji huyo huenda sasa kukayeyushwa.
Chelsea walilipa £23.5 milioni kumchukua Mata kutoka kwa Valencia 2011 na amechaguliwa mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo ya London kwa misimu miwili mfululizo.