EZEKIEL KAMWAGA KATIBU MKUU MPYA SIMBA, MUHAJI AFISA HABARI.

MWENYEKITI wa Simba SC, Alhaj Ismail Rage anatarajiwa kumtaja Ezekiel Kamwaga kuwa Katibu mpya wa klabu hiyo, nafasi iliyoachwa wazi na Evodius Mtawala aliyejiuzulu baada ya kuteuliwa Shirikisho la SOka la SOka Tanzania (TFF).

Aidha, mbunge huyo wa Tabora Mjini CCM, atamtaja pia Mwandishi mwandamizi wa magazeti ya Bingwa na Dimba, Asha Muhaji kuwa Ofisa Habari mpya wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, nafasi ambayo inaachwa wazi na Kamwaga anayepanda cheo.

Habari kutoka ndani ya Simba SC, zimesema kwamba Rage atakuwa na Mkutano na Waandishi
wa Habari mchana wa leo Dar es Salaam kutaja wateuliwa hao wapya.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI