MSANII WA BONGOFLEVA MATATANI KWA DAWA ZA KULEVYA TANGA.
MSANII wa muziki wa kjizazi kipya anayevuma sana kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa Christopher Mhenga maarufu Mkola Man (Pichani) ameingia kwenye mzozo mwingine safari hii akihusishwa na matumizi ya dawa za kulevya na kupelekea kutengwa na baadhi ya marafiki Mambo Uwanjani imeelezwa.
Akizungumza na mtandao huu mara baada ya kuulizwa na mwandishi wa habari hizi kama kweli alifumwa akijidunga dawa hizo za kulevya, Mkola Man alikanusha vikali na kudai yeye atumii kabisa dawa hizo isipokuwa sigara tu.
'Mimi situmii kabisa dawa za kulevya nashangaa kusikia taarifa hizo kuwa natumia dawa, unajua tangia nimeanza kupata umaarufu kupitia wimbo wangu wa Kilevi changu vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii vimekuwa vikiniandika tofauti', aliendelea kulalamika.
Alidai kuwa hivi karibuni alihusishwa na kujiunga na dini ya kishetani ya freemason ambapo imefikia hatua familia yake imemtenga, ameendelea kusema kuwa jamii isimfikirie vibaya na yeye ni mtu safi anayehitaji ushirikiano na watu ili kutimiza malengo.
Amedai anapigana kwa nguvu zote kupinga dawa za kulevya na anashangaa kuona anatajwa kati ya watu wanaotumia wakati yeye anayapinga, ingawa ni msanii na kazi yake kuelimisha jamii bila shaka atasimama mstari wa mbele kupinga, aidha Mkola Man amepanga kukanusha vikali juu ya kuhusika kwake na kundi l,a freemason