OSCAR AIBEBA CHELSEA IKIIADHIBU STOKE.

Bao maridadi kutoka Oscar liliiongoza Chelsea kuwalaza Stoke City 1-0 katika raundi ya nne ya kombe la FA jana Jumapili.

Kiungo huyo wa Brazil ambaye alichukua nafasi ya Juan Mata, aliyesajiliwa na Manchester United, kama kielelezo cha mashambulizi, alitia kimiani kutokana na mkwaju wa adhabu.

Ubora wa bao lake nyota huyo lilidhihirisha sababu iliyomfanya meneja Jose Mourinho kuekeza imani naye na kumruhusu Mata kuondoka Stamford Bridge siku mbili zilizopita.


Chelsea walipoteza nafasi kadhaa za kuadhibu Stoke huku wakipata ulingo wa lango mara mbili lakini hatimaye, wageni wao hawakutishia kulazimisha wenyeji mechi ya marudiano.

“Bao moja kwa bila haitoshi kuonesha jinsi tulivyocheza na kumiliki mechi. La muhimu ni kushinda na kuepuka mchuano wa marudio kwani hatuhitaji mechi ya ziada,” Mourinho aliambia runinga ya ITV.

Meneja wa Stoke, Mark Hughes, alilalamikia uamuzi wa mkwaju wa adhabu dhidi ya Erik Pieters baada ya kukabiliana na straika, Samuel Eto’o, ambao Oscar alifunika wavuni lakini aliinuliwa moya na jinsi vijana wake walivyo cheza.

“Hatukubuni nafasi wazi. Ilikuwa ngumu kwetu lakini ninafurahia yale tuliyoyafanya. Hatukuzama nah ii ni ishara ya mazuri,” aliendelea.

Wachezaji wenye uzoefu miongoni mwao nahodha John Terry na kipa Petr Cech walipumzishwa ingawa Eto’o alipewa nafasi ya kuanza na Mourinho huku Demba Ba, aliyetarajiwa kuorodheshwa akibaki kwenye benchi.

Ni bidii za nyota huyo wa Cameroon aliyefunga matatu dhidi ya United wiki iliyopita ambazo zilifungua ngome ya Stoke na kumruhusu Oscar kuibuka shujaa katika dakika ya 27 pale alipochezewa vibaya na Pietersen.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA