WENGI WATAKUJA MAN UNITED BAADA YA MATA- MOYES

Meneja wa Manchester United, David Moyes, amesema jana kuwa kuvunja rekosi ya timu hiyo kumsajili Juan Mata kutoka Chelsea ndio mwanzo wa kuwasaini wachezaji wengi mwaka huu.

United walikamilisha biashara ya kumleta Mata kwa pauni milioni 37.1 iliyogharimu zaidi kuliko pauni milioni 30.75 walizotoa kumsajili Dimitar Berbatov kutoka Tottenham Hotspur mwaka wa 2008.

Moyes anatarajia Mata atasaidia kusitiri musimu ambao umeshuhudia mabingwa hao wa Ligi ya Premier wakifuata viongozi wa sasa Arsenal kwa alama 14 na kuondolewa kwenye vikombe viwili vya taifa hilo.

United wanakisiwa kuanzisha majadiliano na nyota Wayne Rooney kutia kidole kandarasi mpya huku Moyes akidhibitisha juhudi za kuimarisha kikosi zitaendelea miezi ijayo.


“Huu ndio mwanzo na wengi watatafuata siku zijazo. Nataka ubora wa Juan uzindue juhusi zetu. Sionelei kwamba tutakuwa na wengine watakao sajiliwa Januari lakini bado ninatafakari kutekeleza hilo,” Moyes aliambia runinga ya timu hiyo, MUTV.

Mata aliwasili mwisho wa wiki iliyoshuhudia United wakichakazwa 3-1 kwenye ligi kabla ya kuondolewa kutoka kombe la League Cup na Sunderland katika semi fainali.

Moyes amesema kukamilisha uhamisho huo umeinua nyoyo Old Trafford na anaweza kumorodhesha kwa mara ya kwanza Jumanne.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA