JESHI LA YANGA NOMA UTURUKI.
Mabingwa wa soka nchini, Yanga, jana walianza rasmi mazoezi wakiwa nchini Uturuki walipokwenda kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu na mashindano ya kimataifa.
Kikosi cha Yanga jana asubuhi kilifanya mazoezi kwenye uwanja uliopo ndani ya Hoteli waliyofikia ya Sueno Beach mjini Antalya.
Akizungumza kwa njia ya simu, Kocha wa timu hiyo, Charles Mkwasa aliyeambatana na timu hiyo alisema kuwa programu yake rasmi ya mazoezi anaianza leo Jumamosi.
Yanga iliondoka nchini juzi Alhamisi ambapo ikiwa huko inatarajiwa kucheza michezo mitatu ya kirafiki dhidi ya timu za huko.
Mkwasa alisema mechi hizo zitawasaidia wachezaji wake kujiweka imara kabla ya ligi kuanza na pia kupata uzoefu wa michezo ya kimataifa.
“Mbali na ligi kuu, pia Yanga inakabiliwa na mashindano ya kimataifa hivyo kambi ya huku itaisaidia sana na nimepewa taarifa kuwa tutacheza michezo mitatu ya kirafiki ambayo kwangu naona ni ya umuhimu sana kwenye maandalizi yetu haya,” alisema Mkwasa.
Mkwasa alisema amefurahi kikosi hicho kupata safari hiyo ambayo itawasaidia kufanya mazoezi ya kutosha na timu kutoka nchi nyingine tofauti na za Afrika.
Alisema wachezaji wote wako imara na wapo kwenye harui nzuri hivyo wana nafasi ya kuzingatia zaidi mazoezi wakiwa huko.
Mkwasa ambaye anaiongoza timu hiyo baada ya kutimuliwa kwa Ernest Brandts na msaidizi wake Frerd Felix ‘Minziro’ alisema mazoezi ya jana asubuhi yalikuwa mepesi kwa ajili ya kuweka mwili vizuri na programu yake itaanza rasmi leo.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Beno Njovu alisema mchakato wa kumpata kocha mkuu bado zinaendelea.
Akizungumza jana alisema wanatarajia kumtangaza kocha wiki ijayo na si jana kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Alisema wao kama viongozi bado wako katika harakati za kutafuta kocha mkuu ambaye atasaidiana na kocha Mkwasa katika kukinoa kikosi hicho cha wanajangwani hao ambacho kwa sasa kipo nchini Uturuki.
Hata hivyo habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema baada ya majina mengi yaliyokuwa yameomba kzi hiyo, uongozi umebekisha majina ya makocha wawili raia wa Serbia na Uholanzi ambapo mmoja wapo atatangazwa kocha wa Yanga.