Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2013

MAN CITY YACHAKAZWA NA ASTON VILLA

Picha
Yaya Toure wa Man City Manchester City wamekosa nafasi ya kuwa miongoni mwa viongozi wa ligi waliposhindwa na Aston Villa 3-2.

KIPSANG AVUNJA REKODI YA BERLIN MARATHON

Picha
Mkenya Wilson Kipsang amevunja rekodi ya dunia ya mbio za Marathon kwa kupunguza sekunde 15 aliposhinda mbio za Berlin mapema jumapili.

KIPUTE ULAYA FILIMBI YAPULIZWA, MESSI NJE WIKI TATU

Picha
Steaua Bucharest  v Chelsea Kundi E: Jumanne Saa 3.45 usiku Steaua imepaa kileleni kwa pionti tatu zaidi katika Ligi Kuu ya Romania, baada ya kuilaza Poli Timisoara mabao 3-0, ambayo yalitiwa kimiani na Federico Piovaccari, Nicolae Stanciu na Adrian Popa. Arsenal v Napoli

ANGALIA JINSI AMRI KIEMBA ANAVYOFANANISHWA NA MESSI

Picha
KIUNGO tegemeo wa Simba SC, Amri Ramadhani Kiemba amepata ugonjwa sawa na ambao unamuweka nje Mwanasoka Bora wa Dunia, Lionel Messi kwa wiki tatu, huo si mwingine ni maumivu ya nyama.

LULU AWAKUNA WAKAZI WA MWANZA

Picha
Mamia ya wakazi wa jijini Mwanza wamekunwa na historia ya maisha ya msanii wa maigizo, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu.

NGASA AITANGAZIA VITA SIMBA, AAPA KUILIZA OKTOBA 20

Picha
Winga Mrisho Ngasa (Pichani) wa Yanga amesema ataendelea kucheza kwa kujituma zaidi ili kukisaidia kikosi chake hicho kipya kufikia malengo na kuweka wazi kwamba amejipanga kuifanyia 'kitu mbaya' Simba katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara itakayochezwa Oktoba 20.

TAMBWE AZIDI KUTIKISA LIGI KUU

Picha
Mshambuliaji Amisi Tambwe (Pichani) jana alifunga goli lake la saba katika mechi tatu wakati alipoiongoza Simba kushinda 2-0 dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

CRISTIANO RONALDO ADHIHIRISHA MSHAHARA WAKE, APIGA MBILI REAL IKIUA

Picha
PAMOJA na kumkosa mchezaji ghali duniani, Gareth Bale, lakini mchezaji anayeliwa mshahara mkubwa zaidi duniani, Cristiano Ronaldo alitosha kuipa pointi tatu Real Madrid usiku huu, baada ya kufunga mabao yote katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Elche.

TP MAZEMBE VITANI TENA OKTOBA 6

Picha
TOUT Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), itaanzia ugenini Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stade Malien ya Mali, Oktoba 6, mwaka huu, kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye mjini Lubumbashi.

MATA AFANANISHWA NA CRISTIANO RONALDO

Picha
Juan Mata  Juan Mata has been urged to follow Cristiano Ronaldo's example and broaden his skill set under Jose Mourinho in order to force his way back into the side, Chelsea assistant coach Steve Holland said on Monday.

SUALEZ AREJEA LIVERPOOL, KUWAVAA MAN UNITED JUMATANO

Picha
Luis Suarez  Buoyed by Luis Suarez's return, Liverpool will visit Manchester United in the League Cup on Wednesday eager to inflict more misery on a team reeling from a brutal derby defeat.

WAMAREKANI WAHUSIKA MLIPUKO WA WESTGATE, VIKOSI VYA KENYA KAMILI

Picha
Hatimaye vikosi vya usalama nchini Kenya vinasema vimelidhibiti jengo zima la Westgate mjini Nairobi, ikiwa ni zaidi ya siku tatu baada ya jengo hilo kuvamiwa na wanamgambo.

OKWI KUREJEA ETOILE DU SAHEL, SIMBA ISUBIRI MAJALIWA........

Picha
SIMBA SC itaamua hatima ya msambuliaji wake wa zamani, Emmanuel Okwi (Pichani) mwishoni mwa mwezi huu kama itamrejesha au la, baada ya kufika kwa tarehe ya mwisho ya klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia iliyomnunua Januari mwaka huu ya kulipa fedha za manunuzi yake, dola za Kimarekani 300,000 zaidi ya Sh Milioni 480.

TAMBWE KUIBUKIA YANGA OKTOBA 20

Picha
Mshambuliaji mpya wa Simba, Mrundi Amisi Tambwe, 'amewatishia nyau' mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga baada ya kuweka wazi kuwa amejipanga kuwafunga kwenye mechi yao ya kwanza ya ligi kuu itakayopigwa Oktoba 20 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

KOCHA AZAM AWATAJA WACHAWI WAKE.........

Picha
Kocha Stewart Hall (Pichani) amesema alimuacha nje ya kikosi cha kwanza cha Azam mfungaji bora wa ligi msimu uliopita, Kipre Tchetche na kiungo bora yosso Salum Aboubakar 'Sure Boy', katika mechi waliyoshinda 3-2 dhidi ya mabingwa Yanga, kwa sababu nyota hao wanaonekana wameridhika na mafanikio ya msimu uliopita na hawajitumi.

YANGA YAACHANA NA NGASA............

Picha
Uwezekano wa winga wa Yanga, Mrisho Ngassa (Pichani) kuonekana Uwanja wa Taifa Jumamosi akiwa amevalia uzi wa kijani na njano wakati timu yake itakapokuwa ikivaana na Ruvu Shooting, sasa ni majaliwa baada ya klabu yake kususa kumlipia faini ya Sh. milioni 45 alizotakiwa kuilipa Simba.

MAGAIDI WA WESTGATE MBIONI KUNASWA, MAKOMANDOO WA KENYA KAMILIGADO

Picha
Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya huku mateka wakinusuriwa. Katika ukurasa huu tutakupasha moja kwa moja matukio yanavyojiri katika jengo la Westgate ambako inaarifiwa vikosi vya usalama vimezingira jengo hilo na hata kudhibiti sehemu ya jengo zima.

BREKING NEWS: BRANDTS ATOWEKA JANGWANI

Picha
Uwezekano wa kocha mkuu wa mabingwa wa soka nchini Yanga Ernie Brandts (Pichani) kuendelea kuikochi timu hiyo huenda ukawa shakani kufuatia kauli yake aliyoitoa jana kwamba anatarajia kubwaga manyanga kutokana na matokeo mabaya inayoendelea kuipata timu yake.

MAN UNITED YALAMBISHWA TOPE ETIHAD, YAPIGWA BAKORA 4

Picha
AIBU. aibu kubwa. Manchester United imefungwa mabao 4-1 na wapinzani wa Jiji, Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad.

MASIKINI BALOTELLI! AKOSA PENALTI YAKE YA KWANZA TIMU YAKE IKILALA

Picha
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amekosa penalti kwa mara ya kwanza maishani mwake wakati AC Milan ikilala 2-1 nyumbani katika mchezo wa Serie A dhidi ya vinara Napoli Jumapili hii.

YANGA, AZAM WAINGIZA MILIONI 138, 188, 000.

Picha
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya wenyeji Azam na Yanga lililochezwa jana (Septemba 22 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 138,188,000.

HATIMAYE HAPPYNESS AMVUA TAJI BRIGITE

Picha
Happiness Watimanywa (19) (Pichani) ameung'arisha mkoa wa Dodoma na Kanda ya Kati usiku wa kuamkia jana wakati alipotwaa taji la urembo la taifa 'Redd's Miss Tanzania 2013' baada ya kuwashinda warembo wengine 29 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

YANGA YAANGUSHIWA KIPIGO CHA SHARUBELA

Picha
M abingwa watetezi Yanga waliendeleza mwanzo mbaya wa msimu wakati walipokumbana na kipigo cha magoli 3-2 kutoka kwa Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.

KAKA AENDELEZA KUFURU YAKE, AKATAA KULIPWA MSHAHARA

Picha
Mchezaji wa kiungo cha kati wa AC Milan Kaka ameitaka klabu yake kutomlipa mshahara wake huku akiendelea kupona kutokana na jereha lake la paja ambalo alilipata wakati wa mchezo wake wa kwanza tangu kujiunga na klabu hiyo.

AZAM KUSHUSHA BUNDUKI ZAKE ZOTE KESHO, YAAPA KUIMALIZA YANGA MAPEMAAA.....

Picha
HABARI njema kwa wapenzi wa Azam FC kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC ni kwamba wachezaji wote tegemeo waliokuwa majeruhi sasa wako fiti kwa asilimia 100.

MAKALA: SUGU, KAIMBE MUZIKI, MJENGONI HAKUKUFAI.........

Picha
LUCKY Dube alikuwa Mwanaharakati wa uhuru nchini Afrika Kusini, Dube (Marehemu) alipigania uhuru wa nchi hiyo iliyokuwa ikitawaliwa kimabavu na makaburu.

AGNES MASOGANGE HURU, KUREJEA NCHINI KWA MBWEMBWE........

Picha
Mtanzania Agnes Gerald, maarufu Masogange, ameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada ya kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya.

SIRI YA KUNYIMWA MPIRA TAMBWE HII HAPA

Picha
Hatimaye shirikisho la kandanda nchini TFF limetoboa siri ya kumnyima mpira mshambuliaji wa Simba Mrundi Amisi Tambwe ambaye alifunga magoli manne kwenye mchezo mmoja ulioisha kwa timu yake ya Simba kuilaza Mgambo Shooting mabao 6-0 katika uwanja wa Taifa.

MISS TANZANIA AZUA MAMBO............

Picha
Miss Tanzania Brigitte Lyimo, 19, leo ataweka historia ya mashindano hayo nchini atakapomaliza muda wake bila kukabidhi taji hilo kwa mshindi mpya, jijini Dar es Salam.

SIMBA YAINGIA MCHECHETO, YATISHWA NA KASI YA MBEYA CITY

Picha
Timu ya Mbeya City ambayo imepanda daraja la ligi kuu ya Bara kwa mara ya kwanza katika historia yake mwaka huu inaweza kuwa inalingana kwa pointi na mabingwa watetezi Yanga ambao waliilazimisha kutoka sare ya 1-1 wiki iliyopita, lakini inakutana na mtihani wake mgumu zaidi leo itakapokuwa mgeni wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa.

MOURINHO AANZA KUANDAMWA, ADAI WAKULAUMIWA NI YEYE

Picha
Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho anasema yeye ndiye anayepaswa kuwajibika kufuatia kipigo cha timu yake ilipochuana na Basel kutoka Uswizi 2-1 katika mechi ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya.

TOTTENHAM YAUA 3-0, DEFOE AFUFUKA

Picha
Mabao mawili ya Jermain Defoe yalichgia ushindi wa 3-0 kwa Tottenham dhidi ya Tromso, bao lingine akifunga Christian Eriksen .

SWANSEA YATAKATA ULAYA, YAIFUMUA VALENCIA KWAKE

Picha
WAKALI wa soka ya kitabuni England, Swansea wameanza vyema Europa League baada ya kuifumua mabao 3-0 nyumbani kwake Valencia iliyomaliza na wachezaji 10.

STEWART HALL KUTIMULIWA AZAM, MOROCCO, BANYAI NAO KUTUPIWA VIRAGO

Picha
Hali si shwari! Vibarua vya makocha watatu Hassan Banyai wa Ashanti United, Hemed Morocco wa Coastal Union na Stewart Hall wa Azam vipo katika hatihati kutokana na mwenendo mbovu wa timu zao katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

MUKANGARA MGENI RASMI REDD'S MISS TANZANIA KESHO

Picha
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika shindano la urembo la taifa mwaka huu 'Redd's Miss Tanzania 2013' litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar se Salaam.

KOCHA YANGA AKATA TAMAA YA UBINGWA

Picha
Kocha msaidizi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, Fred Felix  Minziro, amesema wana kazi kubwa kutetea ubingwa huo msimu huu kutokana na timu nyingi zinazoshiriki ligi hiyo kujiandaa vizuri.

AMISI TAMBWE AZITISHA YANGA, MBEYA CITY

Picha
Baada ya kufunga mabao manne katika ushindi wa 6-0 Simba iliyoupata dhidi ya Mgambo JKT juzi, mshambuliaji wa timu hiyo, Mrundi Amisi Tambwe (Pichani) ametamba kuendelea kufumania nyavu Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ikiwano mechi dhidi ya Yanga.

TANZANIA YAMTOSA BALOZI WA UJERUMANI, KISA CHA KUTOSWA ANGALIA HAPA ..........

Picha
Tanzania imemkataa Balozi mteule wa Ujerumani ambaye alitakiwa kuja kufanya kazi nchini.

HAIJAWAHI KUTOKEA, TAMBWE AWEKA REKODI MPYA

Picha
Abdi Kassim 'Babbi' ndiyo mchezaji wa kwanza kufunga goli kwenye uwanja wa Taifa wakati timu ya taifa, Taifa Stars ilipocheza mchezo wa ufunguzi wa uwanja huo dhidi ya timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes', Babbi alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika uwanja huo mpya kabisa.

LICHA YA KUSHINDA 6-0, SIMBA YASHINDWA KUVUNJA REKODI YA YANGA

Picha
MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Simba SC na Mgambo Shooting Stars iliyochezwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeingiza Sh. 58,365,000.

ABEL DHAILA AMSUTA JUMA KASEJA

Picha
KIPA Mganda wa Simba SC, Abbel Dhaira ameonekana kuimarika baada ya kudaka mechi tatu mfululizo bila kuruhusu hata bao moja katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara- hali ambayo inaweza kuwafanya wapenzi wa timu hiyo wasahau kuhusu Juma Kaseja.

BAADA YA KUTOKA SARE MFULULIZO, MGOGORO MKUBWA KUIBUKA YANGA

Picha
WANACHAMA na wapenzi wa Yanga SC walioongozana na timu mjini hapa, wameanza kukata tamaa juu ya mwenendo wa timu hiyo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya sare tatu mfululizo, wakisema mambo mawili makubwa, wachezaji kutojituma na mgawanyiko ndani ya uongozi.

MOURINHO AANZA VIBAYA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Picha
MECHI nne bila ushindi. Kama Rafa Benitez angekuwa bado yupo kazini, angerushiwa mayai viza.

ARSENAL YACHINJA UGENINI, YAIFUMUA MARSEILLE

Picha
ARSENAL imeanza vyema Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Marseille Uwanja wa Velodrome, Ufaransa.

BREKING NEWS: NGASA AKUMBANA NA ADHABU NYINGINE TFF

Picha
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeshindwa kutambua rufani ya Yanga kupinga adhabu ya Mrisho Ngassa kufungiwa mechi sita na kulipa faini ya Sh45 milioni, pamoja na ile ya kutaka mechi yao dhidi ya Mbeya City irudiwe.

PRISONS YAAPA KUFIA UWANJA WA SOKOINE LEO

Picha
Maafande wa jeshi la magereza Tanzania Prisons ya Mbeya leo wameapa kufia katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya watakapokutana na mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga katika mchezo wa mzunguko wa nne wa ligi kuu.

TFF YAZITUHUMU YANGA, MBEYA CITY KUENDEKEZA USHIRIKINA

Picha
Vitendo vivyoashiria imani za kishirikina ambavyo vilidaiwa kujitokeza katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga, vimeziponza timu hizo.

OTTO ADDO AWA MKUFUNZI MPYA HUMBURG

Picha
Addo aliwahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa Ghana Aliekua mchezaji wa timu ya taifa ya Ghana Otto Addo ameteuliwa kua kocha mwenza wa klabu ya Hamburg ya Ujerumani kwa kipindi cha mpito baada ya klabu hiyo kumpiga kalamu kocha wao Thorsten Fink.

JUMA KASEJA, AMANI SIMBA WAIBUKIA ASHANTI UNITED

Picha
NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Juma Kaseja (Pichani) amejiunga na timu ya Ashanti United ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na anatarajiwa kuanza kuichezea rasmi Januari mwakani, baada ya kuchelewa dirisha la usajili.

RONALDO, BALE WANG'ARA, MADRID IKIIUA GALATASARAY YA DROGBA 6-1

Picha
NYOTA Gareth Bale ametokea benchi na kuipikia mabao mawili Real Madrid ikiitandika Galatasaray mjini Istanbul mabao 6-1 huku Cristiano Ronaldo akipiga hat-trick yake ya 21 Bernabeu.