MISS TANZANIA AZUA MAMBO............
Miss Tanzania Brigitte Lyimo, 19, leo ataweka historia ya mashindano hayo nchini atakapomaliza muda wake bila kukabidhi taji hilo kwa mshindi mpya, jijini Dar es Salam.
Brigitte atashindwa kuvua na kukabidhi taji lake kwa mrithi atakayepatikana baada ya wasichana 30 kuchuana kumpokea nafasi hiyo kutokana na kuwa nchini Indonesia ambako Jumamosi atashiriki shindano la kumpata Miss World.
Tangu kuruhusiwa tena kwa mashindano hayo nchini mwaka 1994 baada kuwa yalipigwa marufuku katika miaka ya 60, washindi wote kuanzia Aina Maeda mpaka Salha Israel mwaka jana walikuwepo kwenye onyesho la Miss Tanzania kukabidhi taji.
Kushindwa kuwapo ukumbini kwa Brigitte, ambaye kwa mujibu wa maelezo yake ni mtoto aliyelelewa na mama pekee, kumetokana na kubadilishwa kwa kalenda ya shindano hilo nchini huku Miss World ikiendelea kushindaniwa katika kipindi kilekile cha mwaka.
Kisiwa cha kitalii cha Bali ndiko kutakakofanyika shindano la Miss World 2013 ambalo litashirikisha wasichana 131.
Shindano hilo linafanyika katika kisiwa hicho ambacho wakazi wake wengi ni wenye asili ya Kihindi kufuatia kupingwa na wakazi wa jijini Jakarta ambako kuna asilimia kubwa ya Waisalamu wenye siasa kali.