PRISONS YAAPA KUFIA UWANJA WA SOKOINE LEO

Maafande wa jeshi la magereza Tanzania Prisons ya Mbeya leo wameapa kufia katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya watakapokutana na mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga katika mchezo wa mzunguko wa nne wa ligi kuu.


Maafande hao ambao bado hawajaonyesha makali yao kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, wanatarajia kuchuana na vikali na Yanga ambao wana machungu ya kupoteza mechi mbili mfululizo ambazo walitoka sare ya kufungana 1-1 na Mbeya City.

Yanga imepania kushinda mchezo wa leo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wake lakini itajikuta ikikabiliana vikali na maafande hao ambao wameapa kurudisha heshima yao ili wapate kushabikiwa na wakazi wa mkoa huo.

Tayari mashabiki wa soka mkoani Mbeya wameipa kisogo timu hiyo kutokana na kushindwa kucheza kandanda la kuvutia, mashabiki wengi wameonyesha kuikubali timu iliyopanda daraja msimu huu ya Mbeya City ambapo katika mchezo wake na Yanga walilazimika kulipiga mawe basi lililopakia wachezaji wa timu ya Yanga.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA