Ruka hadi kwenye maudhui makuu

BREKING NEWS: BRANDTS ATOWEKA JANGWANI

Uwezekano wa kocha mkuu wa mabingwa wa soka nchini Yanga Ernie Brandts (Pichani) kuendelea kuikochi timu hiyo huenda ukawa shakani kufuatia kauli yake aliyoitoa jana kwamba anatarajia kubwaga manyanga kutokana na matokeo mabaya inayoendelea kuipata timu yake.


Kwa mujibu wa chanzo chetu chenye uhakika na habari hiyo kimesema kwamba kocha wa Yanga Ernie Brandts amekalia kuti kavu na anasubiri ruhusa tu toka kwa viongozi wakuu, hata hivyo chanzo hicho kinasema kwamba viongozi wa Yanga bado wanamuhitaji Brandts lakini yeye mwenyewe haoini sababu ya kusalia Yanga.

'Timu haifanyi vizuri chini ya utawala wangu ni bora niondoke', kilisema chanzo hicho kikimnukuuu Brandts, Inasemekana Yanga ina mpango wa kumuajiri kocha mzawa kama ilivyofanya Simba kwa sababu haioni tena umhimu wa kuchukua mzungu.

Chanzo hicho kinachoaminika sana kwa habari zake za ukweli kimeendelea kusema kuwa kuna kamgomo baridi kametengenezwa ili kumuondoa Brandts ambaye amekuwa na upendelea katika upangaji wake wa kikosi cha kwanza huku baadhi ya wachezaji muhimu wakiwekwa benchi na kupelekea matokeo mabovu.

Pia baadhi ya viongozi wa Yanga ambao kwa sasa wamewekwa kando wanaendesha kampeni hiyo ya kumng'oa Brandts ambaye aliipa ubingwa wa bara Yanga msimu uliopita, Yanga imejikuta ikipepesuka msimu huu baada ya kuambulia pointi sita zilizotokana na kushinda mechi moja sare tatu na kufungwa moja

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa