RONALDO, BALE WANG'ARA, MADRID IKIIUA GALATASARAY YA DROGBA 6-1

NYOTA Gareth Bale ametokea benchi na kuipikia mabao mawili Real Madrid ikiitandika Galatasaray mjini Istanbul mabao 6-1 huku Cristiano Ronaldo akipiga hat-trick yake ya 21 Bernabeu.


Bale aliwashuhudia Isco, Karim Benzema na Ronaldo wakiiweka klabu yake mbele kwa mabao 3-0 kabla ya kuingia na kutoa mchango wake kunenepesha ushindi.

Kwanza, ilikuwa mpira wa adhabu wa winga huyo wa Wales uliomkuta Ronaldo, ambaye akaifungia bao la nne timu ya Carlo Ancelotti. Kisha akampa pasi Ronaldo, ambaye alimpasia pia Benzema kabla ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kufunga bao lake la pili katika mchezo huo.

Isco alifunga dakika ya 33, Benzema 54 na 81 Ronaldo 63, 66 na 90, wakati bao la kufutia machozi la wenyeji lilifungwa na Bulut dakika ya 84.
Didier Drogba alicheza kwa dakika 45 tu kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Amrabat.

Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas/Lopez dk14, Carvajal, Ramos, Pepe, Arbeloa, Modric/Illarramendi dk72, Khedira, Di Maria, Isco/Bale dk64, Ronaldo na Benzema.

Galatasaray: Muslera, Eboue, Chedjou, Nounkeu, Riera, Inan, Melo, Baytar/Bruma dk62, Yilmaz, Sneijder na Drogba/Amrabat dk46.
Match ball's mine: Cristiano Ronaldo put the ball inside his shirt after netting a hat-trick in Istanbul.

Katika mechi nyingine, Man Utd imeshinda  4 -2 dhidi ya Bayer Leverkusen, Real Sociedad imefungwa nyumbani 2-0 na Shakhtar Donetsk, FC Copenhagen imetoa  1 - 1 na Juventus, Benfica imeifunga 2 - 0  Anderlecht, Olympiacos imefungwa 4-1 nyumbani na  PSG, Bayern Munich imeichapa 3 - 0 CSKA Moscow wakati Plzen imefungwa 3-0 nyumbani na Man City.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA