STEWART HALL KUTIMULIWA AZAM, MOROCCO, BANYAI NAO KUTUPIWA VIRAGO
Hali si shwari! Vibarua vya makocha watatu Hassan Banyai wa Ashanti United, Hemed Morocco wa Coastal Union na Stewart Hall wa Azam vipo katika hatihati kutokana na mwenendo mbovu wa timu zao katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Ashanti United imetangaza kumsimamisha kocha wake Banyai ikiwa ni mwezi mmoja tangu walipoingia naye mkataba wiki moja kabla ya kuanza kwa ligi Agosti 24.
Katibu wa Ashanti United, Abubakari Silas alithibitisha kuwa klabu hiyo imemsimamisha Banyai na hayupo katika kikosi kilichokwenda Kagera kuivaa Kagera Sugar na jana hakuwapo katika mechi ya juzi wakati Ashanti ilipocheza dhidi ya Azam.
Naye meneja wa Ashanti, Mbaraka Hassan alisema wameamua kumsimamisha kocha huyo kufuatia matokeo mabaya ya timu, ambapo kikosi hicho kitakuwa chini ya kocha msaidizi Hassan Ibrahim.
“Kwa sasa kuanzia mchezo wetu na Azam timu ilikuwa chini ya kocha msaidizi baada ya mapendekezo ya uongozi kumsimamisha kwa muda Banyai, siyo kama amefukuzwa bali tunafuatilia kwa ukaribu maendeleo ya timu, atarudishwa wakati wowote uongozi utakapoafikiana,” alisema Mbaraka.
Kocha Banyai hakuwapo kwenye benchi wakati Ashanti ikipata pointi yake ya kwanza msimu huu baada ya kulazimisha sare 1-1 na Azam kwenye Uwanja wa Chamazi uliopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Upepo huo mbaya umepita, pia kwa Azam ambayo lengo lao la kutwaa ubingwa limeanza kwenda kombo baada ya mechi nne ilizocheza kwenye ligi na kushinda moja tu dhidi ya Rhino Rangers na kuambulia sare tatu dhidi ya Ashanti United, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi sita.
Uongozi wa timu hiyo umekasirishwa na matokeo hayo na juzi waliitisha kikao cha dharura na kocha Hall kujadili mwenendo huo.
Baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ashanti, kocha Stewart Hall alikataa kuzungumza na gazeti hili akisema,”nawahi kwenye kikao, kwa sasa sina muda wa kuzungumza na mwandishi.”
Jitihada zilizofanywa kufuatilia kilichojiri kwenye kikao hicho cha dharura ziligonga mwamba baada ya simu za viongozi wa klabu kuita bila kupokelewa.
Ingawa Ofisa habari wa Azam FC, Jafar Iddi alipatikana kwenye simu, lakini aligoma kusema lolote na kujitetea kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu kuwa yuko darasani hawezi kupokea simu.