LULU AWAKUNA WAKAZI WA MWANZA

Mamia ya wakazi wa jijini Mwanza wamekunwa na historia ya maisha ya msanii wa maigizo, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu.


Lulu alikuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa jijini hapa juzi, Jumamosi katika kampeni ya Tambua Fursa Itumie iliyofanyika katika Ukumbi wa Gold Crest jijini hapa.

Msanii huyo aliwataka vijana kutambua fursa walizo nazo na kuzitumia ipasavyo jambo ambalo linaweza kubadili maisha yao kwa jumla.

Alisema tatizo kubwa kwa wazazi huwa hawataki kuwaruhusu watoto wao kutumia fursa walizo nazi na wanazozipata katika maisha yao ya kila siku na badala yake kuwalazimisha kufanya mambo ambayo ni tofauti na kile wanachokitaka.

Akielezea namna alivyozama katika maigizo, Lulu alisema alitambua fursa yake katika kuigiza kabla ya kumtafuta msanii aliyemwona kama mfano wake wa kuigwa katika sanaa hiyo.

"Nilivutiwa na msanii wa Kundi la Kaole anayejulikana kwa jina la Dk. Cheni, huyu alikuwa mfano wangu wakuigwa katika fursa niliyoitambua katika maisha yangu. Hivyo sikupoteza muda kabla ya kumtafuta na kumuomba mwongozo," alisema Lulu.

"Hata hivyo, baada ya kumtafuta Dk. Cheni, alinitaka nimshirikishe kwanza mama yangu mzazi ambapo naye alitoa ushirikiano katika fursa yangu, hivyo, wazazi msiwazuie watoto wenu pindi wanapotambua fursa zao."

Katika semina hiyo pia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba walichangia mada.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA