BREKING NEWS: NGASA AKUMBANA NA ADHABU NYINGINE TFF

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeshindwa kutambua rufani ya Yanga kupinga adhabu ya Mrisho Ngassa kufungiwa mechi sita na kulipa faini ya Sh45 milioni, pamoja na ile ya kutaka mechi yao dhidi ya Mbeya City irudiwe.


Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF chini ya Mwenyekiti Alex Mgongolwa ilimfungia Ngassa baada ya kubaini winga huyo alisaini mkataba wa mwaka mmoja Simba kabla ya kutua Yanga.

Kamati hiyo ilimfungia mechi sita na kulipa faini Sh15 milioni na kuwarudishia Simba Sh30 milioni.

Yanga iliandika barua kwa TFF kukata rufaa ya kupinga adhabu hiyo ingawa kwa sasa shirikisho hilo limewajibu halitambui barua hiyo ni ya kamati ipi ya rufani.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura ameliambia gazeti hili jana jijini Dar es Salaam: “Nafikiri Kamati za Rufani TFF ni nyingi, wao Yanga katika barua yao hawajaeleza wamekata rufaa hiyo kwenye kamati gani.

“Tulichowajibu ni kwamba hatutambui kuwa barua hiyo ya kukata rufaa wameiandikia kamati gani ya rufani TFF,” alisema Wambura.

Naye Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema: “TFF wametujibu kwa maandishi kwamba hawajui rufaa waipeleke kwenye kamati ipi. Ni jambo ambalo limetushangaza kwa kweli.

“Kwa sasa sina cha kukueleza zaidi, naomba usubiri uongozi ukutane kwa ajili ya kulizungumzia hilo,” alisema Baraka.

Mechi kutorudiwa

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeiweka pembeni rufani iliyowasilishwa na Yanga kutaka mchezo dhidi yao na Mbeya City uliofanyika mwishoni mwa wiki  kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya urudiwe.

Uongozi wa Yanga ulifikia hatua hiyo ya kupeleka rufaa TFF, baada ya vuguru zilizotokea kabla ya kuanza kwa mechi na watu wanaodhaniwa kuwa ni mashabiki wa Mbeya City kulipiga mawe basi la Yanga na kumsababisha majeraha dereva wa basi hilo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA