NGASA AITANGAZIA VITA SIMBA, AAPA KUILIZA OKTOBA 20
Winga Mrisho Ngasa (Pichani) wa Yanga amesema ataendelea kucheza kwa kujituma zaidi ili kukisaidia kikosi chake hicho kipya kufikia malengo na kuweka wazi kwamba amejipanga kuifanyia 'kitu mbaya' Simba katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara itakayochezwa Oktoba 20.
Ngasa alilazimika kuwalipa Simba Sh. milioni 45 (Sh. milioni 30 alizochukua ili kusaini kuichezea klabu hiyo na Sh. milioni 15 za fidia), jambo lililofanya licha ya kuitumikia bado "imekula kwake" na Simba ndiyo iliyonufaika.
Wakati akiendelea kuuguza machungu ya kulipa mamilioni hayo, Ngasa anataka kufidia maumivu yake dhidi ya Simba kwa kutumia mpira uwanjani.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mechi yao ya juzi waliyoshinda 1-0 dhidi ya 'maafande' wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana, Ngasa alisema kuwa ana deni kwa mashabiki wa Yanga, hasa baada ya kukosa mechi sita za timu yao ikiwamo ya Ngao ya Hisani walioshinda 1-0 dhidi ya Azam na tano za ligi kuu baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka (TFF).
Ngasa, ambaye juzi alitoka kifungoni na kutoa pasi ya mwisho ya goli pekee la mechi lililofungwa na mshambuliaji Mganda Hamis Kiiza, alisema anaisubiri kwa hamu mechi yao dhidi ya Simba ili 'kumaliza hasira zake' za zilizotokana na kuamuliwa kulipa mamilioni ya fedha.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilimfungia mechi sita mzaliwa huyo wa jiji la Mwanza na kumtaka alipe Sh. milioni 45 baada ya kubaini kuwa aliingia mkataba na Simba kwa ajili ya kuitumikia il-hali bado alikuwa na mkataba na Azam.
Hata hivyo, hukumu hiyo ililalamikiwa kwamba ilitolewa kisiasa kwa maelezo kwamba Simba pia ilipaswa kuadhibiwa kwa kuhusika katika jambo hilo, kwa kumsainisha mkataba mchezaji ambaye ilitambua kuwa alikuwa bado ana mkataba na timu nyingine wakati walipomchukua kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Azam.
Baada ya kutoa pasi ya goli la ushindi juzi, Ngasa alikwenda jirani na jukwaa la Simba na kuanza kuwapungia mikono 'Wanamsimbazi', ishara ambayo alisema kuwa inamaanisha ameanza kazi na wajiandae kwa kipigo Oktoba 20.
"Nina deni kubwa kwa mashabiki wa Yanga, namshukuru Mungu nimemaliza adhabu na leo (juzi) nimetoa pasi ya goli... Simba wajiandae tutakapokutana nao tutawaonyesha kazi," alisema Ngasa ambaye katika mechi ya juzi alicheza vizuri licha ya kuwa nje ya uwanja tangu kuanza kwa ligi hiyo inayodhaminiwa na Vodacom Agosti 24.