MAN UNITED YALAMBISHWA TOPE ETIHAD, YAPIGWA BAKORA 4

AIBU. aibu kubwa. Manchester United imefungwa mabao 4-1 na wapinzani wa Jiji, Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad.


Kocha David Moyes amekaribishwa vizuri na Manuel Pellegrini kwa mabao ya Sergio Aguero dakika ya 16 na 47,  Yaya Toure dakika ya 45 na Samir Nasri dakika ya 50.

Wayne Rooney alitengeneza heshima binafasi kwa bao lake la kufutia machozi aliloifungia United dakika ya 78.

Kikosi cha Manchester City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Jesus Navas /Milner dk71, Toure, Fernandinho, Nasri, Aguero/Javi Garcia dk86 na Negredo/Dzeko DK75.

Manchester United: De Gea 5, Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra, Carrick, Fellaini, Valencia, Rooney, Young/Cleverley DK51 na Welbeck.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA