MASIKINI BALOTELLI! AKOSA PENALTI YAKE YA KWANZA TIMU YAKE IKILALA

MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amekosa penalti kwa mara ya kwanza maishani mwake wakati AC Milan ikilala 2-1 nyumbani katika mchezo wa Serie A dhidi ya vinara Napoli Jumapili hii.


Balotelli, ambaye amefunga penalti zake zote 21 za awali katika mechi rasmi, alishuhudia mkwaju wake ukiokolewa na kipa Pepe Reina dakika ya 60.

Hata hivyo, 'Supermario' aliifungia Milan dakika ya 90 na ushei kabla ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje mwishoni mwa mchezo. Mabao ya Napoli yalifungwa na Britos dakika ya sita na HiguaĆ­n dakika ya 54 pasi ya Zuniga.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA