HAIJAWAHI KUTOKEA, TAMBWE AWEKA REKODI MPYA

Abdi Kassim 'Babbi' ndiyo mchezaji wa kwanza kufunga goli kwenye uwanja wa Taifa wakati timu ya taifa, Taifa Stars ilipocheza mchezo wa ufunguzi wa uwanja huo dhidi ya timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes', Babbi alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika uwanja huo mpya kabisa.


Lakini mshambuliaji mpya hatari raia wa Burundi Amisi Tambwe (Pichani) jana aliandika rekodi mpya pengine haijawahi kutokea baada ya kupachika magoli manne mguuni kwake na kuweza kuandika historia nyingine katika uwanja huo.

Tambwe aliyesajiliwa hivi karibuni akitokea Vital'O ya Burundi aliibuka mfungaji bora wa michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati iliyofanyika Darfur Sudan, pia ndiye mfungaji bora wa ligi ya kwao Burundi, hivyo jana alidhihirisha kwamba hakubahatisha.

Rekodi yake aliyoianza jana itamfanya aendelee kukumbukwa mpaka pale itakapokuja kuvunjwa, hii sasa ni kali kwani washambuliaji kama Jerry Tegete, Kipre Tchetche na wengineo ambao wamezitumikia klabu zao kwa kipindi kirefu lakini wameshindwa kufunga magoli manne katika mechi moja

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA