KIPUTE ULAYA FILIMBI YAPULIZWA, MESSI NJE WIKI TATU

Steaua Bucharest  v Chelsea

Kundi E: Jumanne Saa 3.45 usiku
Steaua imepaa kileleni kwa pionti tatu zaidi katika Ligi Kuu ya Romania, baada ya kuilaza Poli Timisoara mabao 3-0, ambayo yalitiwa kimiani na Federico Piovaccari, Nicolae Stanciu na Adrian Popa.
Arsenal v Napoli

Kundi F: Jumanne Saa 3.45 usiku
Mabao mawili ya Goran Pandev yameipa Napoli pointi tatu dhidi ya Genoa na kupaa kileleni mwa Ligi Kuu Italia, Serie A. Wanalingana kwa pointi na Juventus, 16 kila timu baada ya mechi sita, lakini wanashika usukani kwa wastani wao mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Kundi H: Jumanne Saa 3.45 usiku

Lionel Messi ataikosa mechi hiyo na kuwa nje kwa wiki tatu nyingine, baada ya kuumia nyama za mguu wake wa kulia.

Mwanasoka huyo bora wa dunia alitolewa wakati timu yake ikhinda 2-0 dhidi ya Almeria Jumamosi muda mfupi tu baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 21, ambalo lilikuwa bao lake la nane msimu huu.

Kundi D: Jumatano Saa 3.45 usiku

Thomas Muller alifunga bao pekee katika mchezo mgumu wakati Bayern Munich ikiifunga Wolfsburg 1-0 na kuendelea kukabana koo na Dortmund kileleni mwa Bundesliga. Wana pointi 19 baada ya mechi saba bila kufungwa hata moja.

Kundi A: Jumatano Saa 3.45 usiku

Shakhtar imepanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ukraine, baada ya Eduardo kuwafungia bao la kusawazisha dakika za lala salama dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Metalurh.

Walikuwa wamekwishalala 2-0 lakini walirudisha moja kupitia kwa Alex Teixeira dakika ya 54 na wakajipatia pointi moja, baada ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal kusawazisha zikiwa zimesalia dakika nane.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA