OTTO ADDO AWA MKUFUNZI MPYA HUMBURG
Aliekua mchezaji wa timu ya
taifa ya Ghana Otto Addo ameteuliwa kua kocha mwenza wa klabu ya Hamburg
ya Ujerumani kwa kipindi cha mpito baada ya klabu hiyo kumpiga kalamu
kocha wao Thorsten Fink.
Addo, ambae ni kocha wa timu ya vijana wa chini ya umri wa miaka 19 wa klabu ya Hamburg atashirikiana na kocha wa timu ya akiba Rodolfo Cardoso.
Otto Addo mbaze ni mzaliwa wa Ujerumani aliichezea Hamburg kwa kipindi kati ya mwaka 2007 na 2008.
Aliiwakilisha Ghana kati ya 1999 na 2006, akifunga jumla ya mabao mawili katika michuano 15 na Black Stars.
Hamburg iliamua kumfuta Think "kwa sababu ya matokeo mabaya ya hivi karibuni".
Taarifa ya klabu hiyo iliongeza kusema "hatuna imani tena kwamba Thorsten Fink ataweza kuleta maguzi yoyot katika matokeo."