KOCHA AZAM AWATAJA WACHAWI WAKE.........
Kocha Stewart Hall (Pichani) amesema alimuacha nje ya kikosi cha kwanza cha Azam mfungaji bora wa ligi msimu uliopita, Kipre Tchetche na kiungo bora yosso Salum Aboubakar 'Sure Boy', katika mechi waliyoshinda 3-2 dhidi ya mabingwa Yanga, kwa sababu nyota hao wanaonekana wameridhika na mafanikio ya msimu uliopita na hawajitumi.
"Kuwa na mafanikio msimu uliopita hakukuhakikishii mafanikio msimu huu," alisema Hall.
Muingereza huyo aliongeza kuwa sare tatu katika mechi nne zilimfadhaisha na aliona kuna tatizo kikosini kwamba baadhi ya wachezaji wanaotegemewa hawajitumi.
"Ndiyo maana nikaamua kuwachezesha yosso na nikawaacha nje Kipre Tchetche na Sure Boy. Wanapaswa kujituma ili kuendelea kupata namba kikosini. Niliwaanzisha vijana kwa sababu najua wana usongo wa kupata mafanikio, wanajituma. Huwezi kucheza kama huna bidii," alisema Hall.
Imani yake kwa yosso ilimlipa Hall, ambaye aliwashuhudia wachezaji waliopandishwa kutoka timu yao ya vijana, winga Farid Musa na mshambuliaji Joseph Kimwaga waking'aa.
Kimwaga (18), ambaye aliingia katika uwanjani katika dakika ya 72 kuchukua nafasi ya yosso mwenzake, Musa, aliifungia Azam goli la ushindi katika dakika ya mwisho ya mchezo.
Matokeo hayo yalizima uteja wa Azam wa mechi nne mfululizo kutoka kwa Yanga, ambayo ilitawala kiasi kikubwa cha mechi ya juzi.
Hall pia aliisifu Yanga kuwa ilicheza vizuri zaidi yao akisema kwamba "timu bora" haikushinda juzi baada ya kuwashuhudia mabingwa hao watetezi wakikosa bahati baada ya mashuti yao mawili kugonga mwamba, huku kipa wa Wanalambalamba, Aishi Manula akifanya kazi ya ziada kuzuia "mvua" ya magoli langoni mwa Azam.