AMISI TAMBWE AZITISHA YANGA, MBEYA CITY
Baada ya kufunga mabao manne katika ushindi wa 6-0 Simba iliyoupata dhidi ya Mgambo JKT juzi, mshambuliaji wa timu hiyo, Mrundi Amisi Tambwe (Pichani) ametamba kuendelea kufumania nyavu Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ikiwano mechi dhidi ya Yanga.
Tambwe aliyetua Simba msimu huu baada ya kuipa Klabu ya Vital'O ubingwa wa Ligi Kuu Burundi pamoja na Kombe la Kagame, alisema kinachoendelea sasa ni kazi ya kucheka na nyavu tu.
Akizungumza katika mahojiano maalum baada ya kumalizika mechi dhidi ya Mgambo JKT iliyopigwa Uwanja wa Taifa juzi, Tambwe alisema ilimchukua muda kabla ya kuufahamu vema mfumo wa timu hiyo, lakini sasa haumsumbui tena.
Alisema licha ya kabla ya juzi kocha Abdallah Kibadeni kumchezesha kwa dakika zote 180 wakati wakishinda 1-0 dhidi ya Oljoro JKT Agosti 28, mwaka huu jijini Arusha, na baadaye kuwamo katika kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, alikuwa hajaushika vema mfumo wa timu hiyo.
Tambwe ambaye kwa sasa anaongoza kwa ufungaji katika ligi hiyo baada ya kufumania nyavu mara nne, huku akifuatiwa na Jerry Tegete wa Yanga na kiungo wa Simba, Haruna Chanongo wenye mabao matatu kila mmoja, hakucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora.
Katika mechi hiyo ya ufunguzi iliyopigwa Uwanja Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na kumalizika kwa sare ya 2-2, Tambwe na Mrundi mwenzake, Gilbert Kaze walizuiwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kutokana na kukosa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
"Nilikuwa sijazoea mfumo wa klabu yangu (Simba) na ligi ya Tanzania ambayo ni ngumu kuzidi ya kwetu (Burundi). Sasa nimeshazoeana na wachezaji wenzangu ndiyo maana nimefunga mabao haya," alisema Tambwe.
"Nafanya mazoezi kwa kujituma, natumai nitafanya vizuri zaidi katika mechi zinazofuata. Licha ya kuibuka na ushindi mnono, Mgambo ni timu nzuri. Nitaendelea kufanya kazi kwa kujituma zaidi ili pia nifunge katika mechi zinazofuata kwani kwa kufanya hivyo nitawapa raha mashabiki wangu na klabu ya Simba."
Msimu uliopita katika Ligi Kuu ya Burundi, Tambwe aliibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao 21 katika mechi 18, na baadaye kufanya hivyo tena kwa kufumania nyavu mara sita kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika mjini Darfur, Sudan na Vital'O kutwaa ubingwa.
Mrundi huyo anatajwa kuwa mrithi sahihi wa Mganda Emmanuel Okwi ambaye aliuzwa Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia msimu uliopita, jambo ambalo lilichangia Simba kupoteza ubingwa kwa mahasimu wao wa jadi, Yanga.