MOURINHO AANZA VIBAYA LIGI YA MABINGWA ULAYA

MECHI nne bila ushindi. Kama Rafa Benitez angekuwa bado yupo kazini, angerushiwa mayai viza.


Jose Mourinho amepata kipigo katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa baada ya Chelsea kuchapwa mabao 2-1 nyumbani na FC Basle.
Oscar alitangulia kuwafungia The Blues dakika ya 45, lakini Salah akasawazisha dakika ya 71, kabla ya Streller kufunga la ushindi dakika ya 82 Uwanja wa Stamford Bridge.

Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Oscar, van Ginkel/Mikel dk75, Lampard/Ba dk76, Willian/Mata dk67, Eto'o na Hazard.

Basle: Sommer, Voser, Schar, Ivanov, Safari, Salah/Xhaka dk88, Diaz, Frei, Stocker/Ajetidk 83, Sio/Delgado dk65 na Streller.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA