MOURINHO AANZA KUANDAMWA, ADAI WAKULAUMIWA NI YEYE

Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho anasema yeye ndiye anayepaswa kuwajibika kufuatia kipigo cha timu yake ilipochuana na Basel kutoka Uswizi 2-1 katika mechi ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya.


Alikua mcheza kiungo Oscar aliyeifungulia Chelsea bahati ya uwezekano wa kushinda mechi hiyo lakini Mohamed Salah akarudisha kabla ya Marco Streller kufunga kwa kichwa bao la ushindi kwa Basel.

"tunaposhindwa sizungumzii wachezaji au mtu binafsi, huzungumzia jukumu langu," alisema Mourinho. "anayewajibika ni mimi."
Samuel Eto'o

Nyota aliyesajiliwa hivi karibuni Samuel Eto'o alianza mechi na mshambuliaji Demba Ba kuletwa baadaye katika kipindi cha pili, huku mshambuliaji mwingine Fernando Torres hakua hata kwenye meza ya wachezaji waliorodheshwa.

Hata hivyo meneja huyo kutoka Ureno alisisitiza kua hana wasiwasi juu ya kikosi chake hususan washambuliaji wake, licha ya ukosefu wa magoli.

"ninawaamini washambuliaji wangu watatu kwa msimu mzima," Aliongezea Mourinho.

Mshambuliaji mkongwe kutoka Cameroon Samuel Eto'o aliyehamia kutoka klabu ya Urussi Anzhi Makhachkala, lakini hakumsumbua golikipa wa Basel Yann Sommer hadi kipindi cha majeruhi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA