KOCHA YANGA AKATA TAMAA YA UBINGWA

Kocha msaidizi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, Fred Felix  Minziro, amesema wana kazi kubwa kutetea ubingwa huo msimu huu kutokana na timu nyingi zinazoshiriki ligi hiyo kujiandaa vizuri.


Akizungumza mara baada ya mchezo wa juzi dhidi ya maafande wa Prisons kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini hapa, Minziro alisema ligi ya msimu huu imeonyesha dalili ya kuwa ngumu zaidi ya msimu uliopita.

“Matokeo ya sare tatu mfululizo tuliyoyapata yanathibitisha hilo. Pamoja na kwamba ligi ndiyo kwanza imeanza, lakini ni wazi kuna dalili zote za ligi kuwa ngumu na tuna kazi kubwa katika kutetea ubingwa wetu,” alisema Minziro.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA