Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2024

Maneno ya Kanye West kwa mtu mweusi

Picha
"Tulizoea kumpuuza Michael Jackson kwa sababu walitufanya tuamini kwamba alikuwa kichaa kisha wakamuua,Anasema Kanye West Wakati mtu mweusi anapopata nguvu nyingi na kukataa kudhibitiwa. watatufanya tuamini mambo mengi anayo yafanya niya ukichaa ili tu waweze kumwangamiza,Michael Jackson alichukiwa kwa sababu alikataa kudhibitiwa kama mimi,Kanyewest anasema walijaribu kumpa dawa zenye sumu ili tu wamuue kama walivyomfanyia Michael Jackson,  Pia amesema Baada ya kuwekewa sumu hiyo aliishiwa Nguvu kabisa na alipowauliza kwanini wamemuwekea Sumu wakasema iliwekwa kwa bahati mbaya. Hawa watu wanataka kunitoa roho najua nikifa watakuja na kusema "Oh..!!!! alikuwa na shida sana,tunamkumbuka,tunapenda muziki wake hakika atakumbukwa milele," Lakini nitakuwa nimekufa na hakutakuwa na mtu wa kufichua siri zao tena ndio Maana nasema kabla,Ukweli ni kwamba Watu weupe hawapendi sisi weusi tuwe na Nguvu Kuliko wao. Ndio maana nasema hivi kwa sauti kubwa kwa sababu ulimwengu unahitaji ...

Clara Luvanga apiga bao, Al Nassr ikiua 3-1 Saudi Arabia

Picha
Nyota Wa Tanzania Clara Luvanga Ameiwezesha Timu Yake Ya Al Nassr FC Ya Saudi Arabia Kupata Ushindi Wa Mabao 3 - 1 Dhidi Ya Al-Ula Katika Mchezo Wa Ligi Kuu Ambao Clara Ametupia Wavuni Goli Moja. Magoli Mengine Mawili Yamefungwa Na Ruth Kipoyi Raia Wa Congo Aliyeingia Kipindi Cha Pili Na Lina Raia Wa Algeria.

Mexime ataka marefa nao wafukuzwe wakiboronga

Picha
Kocha wa Dodoma Jiji FC ya jijini Dodoma, Mecky Mexime amewashauri TFF kuwafukuza marefa wanaoboronga kama wanavyofutwa kazi wao makocha. “Mpira hapa umechezwa wewe mwenyewe umeona vuta nikuvute, lakini vitu kama vile vinashusha thamani yetu, mbona sisi tukifanya vibaya tunafukuzwa kwenye timu, sasa wenye mamlaka kama watu wanafanya vibaya kwa nini wasiwafukuze inashindikana kitu gani ee.” "Kama hivi ndo maana makocha wazawa tunadharaulika na hawa wageni wanakuja kuchukua hela na Kuondoka" Mecky Maxime Kocha wa Dodoma jiji baada ya mchezo v Simba SC kuhusu waamuzi.

Camara aitwa tena timu ya taifa

Picha
Golikipawa Simba Sports Club, Moussa Pinpin Camara ameitwa timu ya taifa ya Guinea kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu AFCON dhidi ya Ethiopia. Guinea dhidi ya Ethiopia mechi ya kwanza itachezwa Oct 12 na mechi ya pili Oct 15,2024. Moussa Camara

FIFA yamfungia Eto'o

Picha
BREAKING NEWS: ET'OO AFUNGIWA Shirikisho la Soka Duniani FIFA limefungia miezi 6 Rais wa Shirikisho la soka nchini Cameroon (FECAFOOT) Samuel Eto'o kutohudhuria michezo yeyote ya timu ya Taifa hilo. Eto'o, ambaye ni Rais wa Shirikisho la kandanda nchini Cameroon tangu 2021, alikabiliwa na mashtaka mawili kutokana na tukio la Kombe la Dunia la Wanawake chini ya miaka 20 nchini Colombia Septemba 11. Kwa mujibu wa kamati ya nidhamu ya FIFA, Eto’o alipatikana kuwa alikiuka vifungu vya 13 (“tabia ya kukera na ukiukaji wa kanuni za uchezaji wa haki”) na 14 (“Utovu wa nidhamu wa wachezaji na viongozi”) ya kanuni za nidhamu za FIFA.

TRA yamzulia utata semaji la CAF

Picha
Meneja wa habari wa klabu ya Simba SC, Ahmed Ally ameomba radhi baada ya kutoa kauli iliyoleta tafrani baada ya kuitaja vibaya Mamlaka ya mapato nchini, TRA. Kwenye mahojiano yangu leo nikitoka Dodoma kurudi Dsm, nilinukuliwa nikisema Misimu iliyopita hatukufanya vizuri kwa sababu baadhi ya Wachezaji walikuwa wameridhika na Mafanikio, hawapambani yaaani wanacheza kama Wafanyakazi wa TRA Mfano wa TRA umeeleweka vibaya kiasi cha kuzua taharuki na kwa mantiki hiyo sina budi kuomba radhi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania na wote waliokwazika na sentensi hiyo, amesema Ahmed Ally.

Yanga kwa mbinde yaifunga KMC 1-0

Picha
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara, Yanga SC, usiku huu imeibuka na ushindi mdogo wa bao 1-0 dhidj ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. Bao lililowapa pointi tatu limefungwa na Maxi Nzengeli dakika ya nne kipindi cha kwanza, huo ni ushindi wa tatu mfululizo kwa mabingwa hao wa bara lakini pia ni ushindi wa pili mdogo zaidi kwa timu hiyo ambayo ilizoeleka kushinda kwa idadi kubwa ya magoli. Mashabiki wa timu hiyo hawana furaha ya kuona timu yao ikipata ushindi mdogo jambo ambalo linawaumiza na kuona msimu huu timu yao inaelekea wapi?

Simba yaendelea kutesa Ligi Kuu bara

Picha
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC usiku huu imeichapa Dodoma Jiji FC bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Goli pekee la Wekundu hao wa Msimbazi limefungwa na Jean Charles Ahoua dakika ya 63 kwa mkwaju wa penalti. Hilo ni bao lake la pili kwa kiungo huyo raia wa Ivory Coast ambaye amekuwa na mwanzo mzuri tangu alipojiunga na kikosi hicho, Simba ikiwa imecheza mechi 4 imefikisha pointi 12

Singida Black Stars yashikwa shati

Picha
Singida Black Star yapunguzwa Kasi na Maafande wa JKT Tanzania baada ya kulazimishwa sare kwenye uwanja wao wa Nyumbani wa Liti. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1 ambapo kwa matokeo hayo ni kama Singida Black Stars imeshikwa shati. Singida Black Stars walitangulia kupata bao kupitia Elvis Rupia dakika ya 16 lakini JKT Tanzania walisawazisha kupitia kwa Wilson Nangu dakika ya 62

Mashujaa FC yaibana mbavu Azam FC

Picha
Timu ya Mashujaa FC jioni ya leo imeilazimisha Azam FC kwenda nayo sare isiyo na mabao 0-0 katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma mchezo wa Ligi Kuu bara. Hali sio nzuri kwa Azam ambao msimu uliopita ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya pili na kushiriki michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika. Kwasasa Azam FC imefikisha pointi 9 ikiwa imecheza mechi 6 lakini kwa jinsi ilivyo sidhani inaweza kuwa kama msimu uliopita

Diarra achomoza Afrika

Picha
Kipa wa Yanga, Djigui Diarra, ameingia anga za makipa bora Afrika akila sahani moja na Sipho Chaine wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwa kucheza mechi nne za hatua ya awali katika Ligi ya mabingwa Afrika bila kuruhusu bao lolote. Makipa hao wawili wametumia dakika 360 za mechi nne za raundi ya kwanza na ya pili bila kuruhusu bao, wakiwafunika hadi Ronwen Williams wa Mamelodi Sundowns na Mohamed El Shenawy wa Al Ahly, ambao wametumika katika dakika 180 kupitia mechi mbili kila mmoja bila kuruhsu bao lolote hadi sasa. Diarra amekuwa nguzo muhimu kwa Yanga, akisaidia timu kufika hatua ya makundi bila kuruhusu goli, jambo linalomweka katika kundi la makipa hao. Diarra ametumia dakika hizo katika mechi mbili za raundi ya kwanza dhidi ya Vital’O Burundi na Yanga ilishinda jumla ya mabao 10-0 ikianza kwa kushinda 4-0 na ziliporudiana ilishinda tena 6-0, kisha ikacheza mechi za raundi ya pili dhidi ya CBE SA ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 7-0. Diarra aliendeleza umwamba kwa kuisaidia Yanga ...

Fiston Mayele atua Real Madrid

Picha
Mshambuliaji wa DR Congo na Pyramids FC Mayele alitembelea Santiago Bernabéu na kupiga picha na kombe la UEFA Champions League. Mayele anaichezea Pyramids ya Misri lakini amewahi kuichezea Yanga SC ya Tanzania na AS Vita Club ya DR Congo

Ugonjwa wa Prof Jay wayabadili maisha ya mke wake

Picha
Mke wa mwanamuziki mkongwe wa Bongofleva Joseph Haule "Prof Jay" amedai ugonjwa wa mumewe umeyabadili maisha yake. "Ugonjwa wa mume wangu umebadili maisha yangu ,mke wa mwanamuziki na mwanasiasa wa upinzani Prof Jay Professo Jay, anasema ni ‘lazima kwa yeye kuishi kama nyota’ huwa inamuwia vigumu sana kutenganisha maisha yake binafsi na maisha ya mume wake.

Poul Pogba anatia huruma

Picha
Nyota wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Poul Pogba ametoa maneno ya kushangaza ambayo aliwahi kuambiwa na baba yake zamani. "Nilipopata mshahara wangu wa kwanza mkubwa kutoka Manchester United nilikuwa na furaha sana na baba akaniambia " mwanangu usichezee pesa maana haya yakiisha watu wote wataondoka na kukuacha mwenyewe". Sikuelewa maneno hayo mpaka nilipopata matatizo ndipo niligundua marafiki waliyonizunguka muda wote hawaji tena kuniona. Watu pekee niliobaki nao ni familia yangu tu. Hayo ndio maisha. " , Alisema Pogba

Aishi Manula kuwa chambo kwa Feitoto kutua Simba

Picha
WAKATI klabu ya soka ya Simba ikikamilisha mipango ya kumnasa winga, Elie Mpanzu, aliyemaliza mkataba na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Simba inatajwa sasa imehamishia nguvu zake kumnasa kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto' huku ikimhusisha kipa, Aishi Manula 'Tanzania One'. Habari zilizopatikana jijini, Dar es Salaam zinasema Simba inataka kubadilishana wachezaji, ikijipanga kumwachia Manula aende Azam ili impate Fei Toto pamoja na fedha. Chanzo chetu kinadai Simba iko tayari kulipa kiasi cha Sh. milioni 350 katika kuhakikisha mchakato huo wa usajili unafanikiwa. Taarifa zaidi zinasema Simba imeamua kutengeneza mtego huo kwa sababu ya mahitaji ya kila timu, ambapo wao wanamhitaji kwa udi na uvumba Fei Toto huku Azam FC ikitaka huduma ya Manula ili kufikia malengo. Chanzo hicho kiliongeza tayari Simba imeanza mchakato wa usajili kutokana na kutinga hatua ya makundi katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo inaruhusiwa...

Tanzania inapaswa kuwa timu 4 kwenye michuano ya vilabu Afrika

Picha
Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon ,Samuel Etoo amesema Mataifa yenye Nguvu kisoka ngazi ya Vilabu kama Tanzania yanapaswa kuwa na Timu 4 Kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho na Klabu Bingwa Afrika. . “Nafikiri ni wakati sahihi kubadilisha mfumo wetu wa upatikanaji wa vilabu katika Mashindano yetu ya CAFCL na CAFCC. . “Tunapaswa kufanya kama wanavyofanya watu wa Ulaya na Asia, Mataifa yenye Ligi zenye nguvu hayapaswi kutoa Timu sawa na Mataifa yenye Ligi dhaifu” . “Mataifa kama Tanzania, Afrika Kusini, Congo DR, Senegal, Misri, Algeria, Morocco, Tunisia na Libya kwasababu wanaligi bora wanapaswa kutoa Timu Nne CAFCL na nyengine Nne CAFCC” . “Endapo tutatumia mfumo huu utasaidia kuleta ushindani zaidi lakini pia kuongezeka kwa mashabiki wanaofuatilia Mashindano haya” . “Kila bara kwasasa duniani linapambana kuongeza ushindani katika mashindano yao ya Vilabu na sisi Afrika tunatakiwa tubadilike kwasababu binafsi naamini sisi Waafrika ni Bora kisoka Duniani kuliko bara Lolote lile.”...

Martinez asimamishwa kwa udhalilishaji

Picha
Mchezaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Aston Villa, Emiliano Martinez, amesimamishwa na Shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA kwa "tabia ya udhalilishaji" na atakosa mechi mbili zijazo za Argentina. Adhabu hiyo imetokana na matukio mawili katika mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026, dhidi ya Chile na Colombia. Martinez alirudia aina yake ya ushangiliaji wa kushika sehemu za siri ambapo alionywa namna hiyo ya ushangliaji tangu fainali ya kombe la Dunia mwaka 2022. Kwa upande wa Shirikisho la Soka Argentina AFA, imeonyesha kutokubaliana na adhabu hiyo kwa mlinda mlango wao namba 1, Hivyo basi kipa huyo mshindi wa tuzo ya kipa bora kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, atakosa mechi za kuwania kufuzu kombe la Dunia kati ya Argentina dhidi ya Venezuela na Bolivia mwezi Oktoba,2024.

Ni marufuku kumjadili mwamuzi hata kama akiboronga

Picha
Bodi ya Ligi (TPLB) kupitia kanuni zinazosimamia ligi hiyo zinazokataza makocha, wachezaji na viongozi kuwajadili waamuzi. Kanuni ya 40 kifungu cha (2) cha Udhibiti wa Kimashindano kinaainisha kuwa: . “Ni marufuku kwa kocha/kiongozi wa timu/klabu, mchezaji au mdau mwingine yeyote wa mpira wa miguu kushutumu au kutoa matamshi/maandiko/picha/video kwa lengo la kumkejeli au kumshutumu au kumkashifu au kumdhalilisha mwamuzi yeyote wa mchezo/kiongozi wa TFF/FA (M)/TPLB kwenye vyombo vya habari na mahali pengine popote. . “Kiongozi au mdau atakayekiuka atafungiwa idadi ya michezo isiyopungua mitatu au kutojihusisha na mpira wa miguu kwa kipindi kati ya miezi mitatu mpaka kumi na miwili na au faini kati ya Sh500,000 hadi 5,000,000. Wallace Karia

Nay wa Mitego alikoroga tena, aitwa BASATA

Picha
Msanii Emmanuel Elibariki, maarufu 'Nay Wa Mitego' anatuhumiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kutoa wimbo wake uitwao NITASEMA bila kibali, kinyume na taratibu za Baraza hilo Pia, Nay Wa Mitego anadaiwa kutoa Wimbo huo wenye maudhui yanayohamasisha uchochezi dhidi ya Serikali, kuipotosha jamii kuhusu uwezo wa Rais kutekeleza majukumu yake na kukashifu mataifa mengine kama Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jambo ambalo linaweza kuleta mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na mataifa hayo Aidha, Hati ya Makosa imesema Wimbo wa 'NITASEMA' ulisambazwa kwa walaji kabla ya kupewa kibali cha kuthibitisha kuwa maudhui yake yamezingatia maadili yanayotakiwa

Fountain Gate yaendeleza vichapo Ligi Kuu bara

Picha
Fountain Gate wanakwea kileleni mwa Msimamo wa NBCPL baada ya kuwachapa Kagera Sugar mabao 3-1 kwenye uwanja wao wa Nyumbani wa Tanzanite Mjini Babati. Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Suleiman Mwalimu, Salum Kihimbwa na Elie Makono, goli la kufuta machozi la Kagera Sugar limefungwa na Obrey Chirwa

Abdul Machela: Sina bahati ya kucheza makundi kombe la Shirikisho

Picha
Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu ya Black Bulls Lichinga ya Msumbiji Abdul Machela raia wa Tanzania ni kama amepishana na bahati baada ya kuihama timu hiyo na kujiunga na timu nyingine. Machela ameihama Black Bulls wakati timu hiyo ikicheza Ligi daraja la kwanza la nchi hiyo na akatimkia klabu nyingine iliyoshiriki Ligi Kuu ya nchini humo. Lakini kilichotokea, kwamba Black Bulls imefanikiwa kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika na imepambana vya kutosha na kuweza kutinga hatua ya makundi. Mtanzania Abdul Machela ambaye baba yake aliwahi kuichezea Simba SC pia ya Tanzania ambayo nayo imetinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika. Machela kwa sasa anaichezea timu ya Real de Cuamba ya nchini humo, Mambo Uwanjani Blog ilizungumza na Machela ambapo amesema haikuwa bahati yake kwani amecheza muda mrefu hajakutana na zari kama hilo. Abdul Machela (wa kwanza ) kulia

Diddy atangaza kuuza mjengo wake wa kifahari

Picha
Ni rasmi sasa rapa, producer na mfanyabishara Sean Combs 'Diddy' anauza mjengo wake uliopo Beverly Hills, California Dola Milioni 61 sawa na Tsh Bilioni 166 na ushee. Mjengo huo aliununua mwaka 2014 dola milioni 39 Tsh Bilioni 106 una vyumba 10, ukubwa wa futi za mraba 17000, ekari 1.3, sebule kubwa, chumba cha chakula, barabara, ukumbi wa michezo, ghorofa 2 za wageni na studio ya kurekodi. Unaambiwa mauzo ya mjengo huo inafanya kuingia orodha ya pili kwa nyumba zilizouzwa kwa bei kubwa zaidi eneo hilo la Beverly Hills.

Chid Benzi aamua kutembea kwa miguu kisa nauli

Picha
Msanii wa Hip Hop, Chid Benz amesema ameamua kutembea kwa miguu kutokana na madereva wengi wa bodaboda kuogopa kumbeba wakidhani hatawalipa nauli zao. Chid maisha yake yamebadilika na mwenyewe amesema anapenda anavyoishi sasa na hata akiwa na hela hatayabadilisha. "Maisha ninayoishi sasa hivi ni mazuri sana,watu wananipita tu hawanishangai, yaani siishi kwa uoga sababu ya watu watanionaje au waandishi wa habari wataniona. "Haya ndiyo maisha ninayoishi na hata nikija kupata pesa niteendelea kuishi hivi, ila kuna hawa waendesha bodaboda huwa wanazingua sana. Yaani nikiwasimamisha kutaka usafiri baadhi yao wanakataa kunipandisha wanadhani sitawalipa pesa," amesema na kuongeza ana uwezo wa kutembea kwa miguu kutoka Sinza hadi Magomeni bila ya kupata usumbufu wowote na maisha yake yote sasa hivi asilimia kubwa anatembea kwa miguu.

Kocha Azam adai magoli yote ya Simba ni off side

Picha
KOCHA wa Azam FC Rachid Taoussi raia wa Morocco amedai magoli yote waliyofungwa na Simba yalikuwa off side na amesisitiza haraka sana iletwe VAR. “Tunahitaji VAR magoli yote mawili ni offside za wazi , Simba ni timu kubwa hilo hatukatai niwapongeze wachezaji wangu lakini kwanini offside ni kwetu tu” Maneno ya Rachid Taoussi kocha mkuu wa Azam FC baada ya kumalizika kwa mchezo. Rachid Taoussi kocha wa Azam FC

Simba ya safari hii haitanii, yaichapa Azam 2-0

Picha
Simba ya safari hii haina utani hata kidogo kwani usiku huu imeichapa Azam FC mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu bara kwenye uwanja wa New Amaan Zanzibar. Lionel Ateba dakika ya 15 aliifungia Simba SC bao la uongozi kabla ya Fabrice Luamba Ngoma dakika ya 47 kufunga la pili. Hata hivyo goli la pili lililofungwa na Ngoma, linadaiwa ni off side lakini waamuzi wa mchezo huo wakiongozwa na Elie Sasii alikubaliana na goli hilo. Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 9 ikiwa imecheza mechi 3 na inazidi kuiacha nyuma Yanga ambayo jana ilipata ushindi kiduchu dhidi ya KenGold .

Wachezaji wangu hawakupata muda wa kupumzika- Gamondi

Picha
Kocha mkuu wa Yanga SC Miguel Gamondi raia wa Argentina,amesema wachezaji wake hawakupata muda wa kupumzika baada ya kutoka kwenye mchezo wa kimataifa. “Jumamosi tulikuwa Zanzibar, Jumapili tukasafiri kurudi Dar, kisha Jumatatu tukasafiri kuja Mbeya jambo ambalo timu imekosa muda mwingi wa kupumzika na kujiandaa kwa mechi," “Ratiba inaonekana ni ngumu, lakini ninaifurahia kwani nina wachezaji wengi wanaoweza kucheza kwa kubadilishana na kufanya vizuri.” Alisema Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Miguel Gamondi

Mzamiru, Kagoma kuikosa Azam

Picha
Nyota wawili wa Simba SC ambao Yusuph Kagoma na Mzamiru Yassin hawatakuwa sehemu ya mchezo wa leo dhidi ya Azam Fc kukotana na majeraha ambayo yanawasumbua. Kauli hiyo imethibitishwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmedy Ally kuwa kukosekana kwa wachezaji kama hao ni pengo kubwa lakini Simba ni timu kubwa na pia inawachezaji wengi.

Kesi ya Masoud Kipanya na Mwijaku yapigwa kalenda

Picha
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar imepanga kusikiliza Mapingamizi manne ya kisheria yaliyowasilishwa na Burton Mwemba (Mwijaku) dhidi ya mashtaka ya kashfa yanayomkabili kutoka kwa Masoud Kipanya, Oktoba 17, 2024 mbele ya Jaji David Ngunyale - Amri ya kuanza kusikiliza mapingamizi hayo kabla ya kesi ya msingi imetolewa na Jaji Ngunyale baada ya kupokea hati ya utetezi ya Mawakili wa Mwijaku, ambapo Wakili wa Kipanya alikubaliana na amri hiyo - Katika pingamizi hilo, Mawakili wa Mwijaku wanaiomba Mahakama ifute kesi ya msingi kwa gharama, wakidai kuna kasoro za Kisheria kama uwezo wa Mahakama kusikiliza kesi hiyo, makosa katika uthibitishaji wa maelezo, na kukosekana kwa vielelezo sahihi - Katika kesi ya msingi, Kipanya anamdai Mwijaku fidia ya Tsh. Bilioni 5.5 kwa kumkashfu kupitia Facebook pamoja na Mitandao mingine ya Kijamii, akihusishwa na biashara haramu na madai ya kuhongwa ili kuwachafua Viongozi wa Serikali, akiwemo Rais Mwijaku (Kushoto), Kipanya (Kulia)

KenGold kufanya sherehe ya kufungwa goli moja na Yanga

Picha
Taarifa iliyopo kwasasa kwamba klabu ya KenGold ya Chunya mkoani Mbeya inataka kufanya sherehe kubwa baada ya kufungwa goli moja na Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliochezwa jana. Msemaji wa timu hiyo Jobe Mkoko ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii. "Kuna watu walianzishwa 1936 lakini walipigwa 7 na Yanga,wengine juzi tu walikufa 6.Sisi kama KENGOLD tutafanya sherehe kufungwa goli moja tu na YangaSc"

Baada ya Mpanzu, Philipe Kinzumbi aitaka Simba SC

Picha
Winga wa klabu ya TP Mazembe, Philippe Kinzumbi ameuambia Uongozi wake wa TP Mazembe kuwa anahitaji kucheza soka katika ukanda wa Afrika Mashariki ( Tanzania ) kuelekea msimu ujao wa 2024/25. Licha ya TP Mazembe kumpa taarifa Philippe Kinzumbi kuwa vilabu vya Club Africain na MC Alger zimepeleka ofa rasmi kwa Kunguru wa Lubumbashi ili kupata huduma ya mchezaji huyo ambaye amekuwa na msimu bora sana lakini amekataa kwenda kucheza soka Uarabuni. Simba Sc Wanaendelea Kufanya Mpango wa Kumpata Lakini pia Baada Yanga kusikia Story zake nao wakaanza Kumfuatilia na mazungumzo na TP Mazembe mwanzoni mwa wiki ijayo ili kuipata saini ya Philippe Kinzumbi na kulingana na uhusiano wa karibu baina ya vilabu hivi viwili basi watakuwa na wakati mzuri wa kumpata Kinzumbi ambaye amekubali kucheza Afrika Mashariki.

HONGERENI YANGA NA SIMBA KWA KUFUZU MAKUNDI

Picha
NA PRINCE HOZA WIKIENDI iliyopita ilikuwa siku ya furaha kws Watanzania hasa baada ya wawakilishi wao Yanga SC na Simba SC kufuzu hatua ya makundi kwenye michuano ya kimataifa. Yanga SC inashiriki michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika wakati Simba SC inashiriki kombe la Shirikisho barani Afrika, timu zote hizo zilifanya vema katika mechi zake zilizofanyika kwenye viwanja vya nyumbani. Ilianza Yanga SC ambao walikutana na mabingwa wa Ethiopia, CBE ambapo katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Abebe Bikila, Yanga ilishinda kwa bao 1-0 ambalo liliwekwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumalelo. Yanga ambao ni mabingwa wa Tanzania bara, walipata ushindi mkubwa katika mchezo wa marudiano uliofanyika Zanzibar katika uwanja wa New Amaan Stadium, ushindi wa mabao 6-0 uliwapeleka moja kwa moja hatua ya makundi. Mabao ya Yanga yalifungwa na Clatous Chama, Clement Mzize, Stephanie Aziz Ki (mawili), Mudathir Yahya na Duke Abuye, jumla Yanga inaingia...

#TupoNaMama: Rais Samia awajengea barabara wanaNyasa

Picha
Rais Samia Suluhu Hassan amefika Wilaya ya Nyasa kwa takribani zaidi ya miaka 14 hakuna Rais aliyewahi kukanyaga huku, Rais Samia amefika pasipofika kwa kuwajengea barabara na huduma za maendeleo.

Yassif Basigi amrithi Mgunda, Simba Queens

Picha
Na Ikram Khamees Timu ya Simba Queens imemtangaza Yussif Basigi (52) kuwa kochs wake mkuu akichukua nafasi ya Juma Mgunda aliyetupiwa virago. Basigi atasaidiwa na Mussa Hassan Mgosi, kipaombele ya cha huyo ni kusajili wachezaji bora kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Ghana anakotokea

Kitasa cha Yanga, atambulishwa ST George

Picha
Beki wa zamani wa klabu ya Yanga SC ,Gift Fred ametambulishwa rasmi katika klabu yake mpya ya St George inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ethiopia. Gift ameachwa na Yanga ili kumpisha Jean Baleke, alikuwa miongoni mwa mabeki wanaounda safu ya ulinzi ya timu hiyo uliochini ya Ibrahim Baka Gift Fred

Yanga yashinda kiduchu

Picha
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC jioni ya leo imeibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya KenGold katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara. Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi 6 na mechi mbili huku ikiendelea kusaka ushindi kwenye mechi ijayo dhidi ya KMC. Bao pekee la Yanga limefungwa na Ibrahim Baka dakika ya 13 kipindi cha kwanza, Krngold ambao kwenye mechi zake imepoteza, lakini leo imejidhatiti na kidogo wasifungwe mchezo huo kwani walilinda mno lango lao. Mashabiki wa Yanga hawakuamini timu yao kubanwa na kuambulia ushindi kiduchu huku wakishindwa kuishusha Simba iliyombele yao