Wachezaji wangu hawakupata muda wa kupumzika- Gamondi
Kocha mkuu wa Yanga SC Miguel Gamondi raia wa Argentina,amesema wachezaji wake hawakupata muda wa kupumzika baada ya kutoka kwenye mchezo wa kimataifa.
“Jumamosi tulikuwa Zanzibar, Jumapili tukasafiri kurudi Dar, kisha Jumatatu tukasafiri kuja Mbeya jambo ambalo timu imekosa muda mwingi wa kupumzika na kujiandaa kwa mechi,"
“Ratiba inaonekana ni ngumu, lakini ninaifurahia kwani nina wachezaji wengi wanaoweza kucheza kwa kubadilishana na kufanya vizuri.”
Alisema Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Miguel Gamondi