Tanzania inapaswa kuwa timu 4 kwenye michuano ya vilabu Afrika
Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon ,Samuel Etoo amesema Mataifa yenye Nguvu kisoka ngazi ya Vilabu kama Tanzania yanapaswa kuwa na
Timu 4 Kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho na Klabu Bingwa Afrika.
.
“Nafikiri ni wakati sahihi kubadilisha mfumo wetu wa upatikanaji wa vilabu katika Mashindano yetu ya
CAFCL na CAFCC.
.
“Tunapaswa kufanya kama wanavyofanya watu wa Ulaya na Asia, Mataifa yenye Ligi zenye nguvu hayapaswi kutoa Timu sawa na Mataifa yenye Ligi dhaifu”
.
“Mataifa kama Tanzania, Afrika Kusini, Congo DR, Senegal, Misri, Algeria, Morocco, Tunisia na Libya kwasababu wanaligi bora wanapaswa kutoa Timu Nne CAFCL na nyengine Nne CAFCC”
.
“Endapo tutatumia mfumo huu utasaidia kuleta ushindani zaidi lakini pia kuongezeka kwa mashabiki wanaofuatilia Mashindano haya”
.
“Kila bara kwasasa duniani linapambana kuongeza ushindani katika mashindano yao ya Vilabu na sisi Afrika tunatakiwa tubadilike kwasababu binafsi naamini sisi Waafrika ni Bora kisoka Duniani kuliko bara Lolote lile.”
Maneno ya Rais wa Shirikisho la Soka Cameroon (FECAFOOT), Samuel E'too akizungumza kupitia Mahojiano na Kituo cha Televisheni cha RTI 1.