Aishi Manula kuwa chambo kwa Feitoto kutua Simba


WAKATI klabu ya soka ya Simba ikikamilisha mipango ya kumnasa winga, Elie Mpanzu, aliyemaliza mkataba na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Simba inatajwa sasa imehamishia nguvu zake kumnasa kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto' huku ikimhusisha kipa, Aishi Manula 'Tanzania One'.

Habari zilizopatikana jijini, Dar es Salaam zinasema Simba inataka kubadilishana wachezaji, ikijipanga kumwachia Manula aende Azam ili impate Fei Toto pamoja na fedha.

Chanzo chetu kinadai Simba iko tayari kulipa kiasi cha Sh. milioni 350 katika kuhakikisha mchakato huo wa usajili unafanikiwa.

Taarifa zaidi zinasema Simba imeamua kutengeneza mtego huo kwa sababu ya mahitaji ya kila timu, ambapo wao wanamhitaji kwa udi na uvumba Fei Toto huku Azam FC ikitaka huduma ya Manula ili kufikia malengo.

Chanzo hicho kiliongeza tayari Simba imeanza mchakato wa usajili kutokana na kutinga hatua ya makundi katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo inaruhusiwa kufanya uhamisho, ingawa uhalali wake utaidhinishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), wakati wa dirisha dogo la usajili.

Feisal Salum "Feitoto"

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA