Yanga kwa mbinde yaifunga KMC 1-0
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara, Yanga SC, usiku huu imeibuka na ushindi mdogo wa bao 1-0 dhidj ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Bao lililowapa pointi tatu limefungwa na Maxi Nzengeli dakika ya nne kipindi cha kwanza, huo ni ushindi wa tatu mfululizo kwa mabingwa hao wa bara lakini pia ni ushindi wa pili mdogo zaidi kwa timu hiyo ambayo ilizoeleka kushinda kwa idadi kubwa ya magoli.
Mashabiki wa timu hiyo hawana furaha ya kuona timu yao ikipata ushindi mdogo jambo ambalo linawaumiza na kuona msimu huu timu yao inaelekea wapi?