Singida Black Stars yashikwa shati
Singida Black Star yapunguzwa Kasi na Maafande wa JKT Tanzania baada ya kulazimishwa sare kwenye uwanja wao wa Nyumbani wa Liti.
Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1 ambapo kwa matokeo hayo ni kama Singida Black Stars imeshikwa shati.
Singida Black Stars walitangulia kupata bao kupitia Elvis Rupia dakika ya 16 lakini JKT Tanzania walisawazisha kupitia kwa Wilson Nangu dakika ya 62