Simba yaendelea kutesa Ligi Kuu bara
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC usiku huu imeichapa Dodoma Jiji FC bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Goli pekee la Wekundu hao wa Msimbazi limefungwa na Jean Charles Ahoua dakika ya 63 kwa mkwaju wa penalti.
Hilo ni bao lake la pili kwa kiungo huyo raia wa Ivory Coast ambaye amekuwa na mwanzo mzuri tangu alipojiunga na kikosi hicho, Simba ikiwa imecheza mechi 4 imefikisha pointi 12