Abdul Machela: Sina bahati ya kucheza makundi kombe la Shirikisho

Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu ya Black Bulls Lichinga ya Msumbiji Abdul Machela raia wa Tanzania ni kama amepishana na bahati baada ya kuihama timu hiyo na kujiunga na timu nyingine.

Machela ameihama Black Bulls wakati timu hiyo ikicheza Ligi daraja la kwanza la nchi hiyo na akatimkia klabu nyingine iliyoshiriki Ligi Kuu ya nchini humo.

Lakini kilichotokea, kwamba Black Bulls imefanikiwa kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika na imepambana vya kutosha na kuweza kutinga hatua ya makundi.

Mtanzania Abdul Machela ambaye baba yake aliwahi kuichezea Simba SC pia ya Tanzania ambayo nayo imetinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika.

Machela kwa sasa anaichezea timu ya Real de Cuamba ya nchini humo, Mambo Uwanjani Blog ilizungumza na Machela ambapo amesema haikuwa bahati yake kwani amecheza muda mrefu hajakutana na zari kama hilo.

Abdul Machela (wa kwanza ) kulia

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA